SamuraiJack
JF-Expert Member
- Dec 24, 2017
- 462
- 740
Habari zenu wakuu? Natumaini wote mpo salama na mnaendelea vizuri.
Nina mtaji ambao ninatarajia kuwekeza katika kufungua barber shop eneo la Msamvu, karibu na Stendi Kuu ya Morogoro. Mpango wangu ni kuwa na viti vinne vya kisasa vya kunyolea, pamoja na chumba maalumu cha scrub chenye vitanda viwili na sinki la kuoshea. Tayari nimefanya makadirio ya gharama zote zinazohitajika, ikiwemo AC, heater ya maji, partition za ndani, pamoja na kupata eneo la biashara.
Niliwahi kumiliki salon ndogo miaka iliyopita, lakini niliiuza kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Mimi si kinyozi, hivyo nilishindwa kuisimamia ipasavyo. Safari hii nimejipanga vizuri zaidi. Pia nimepanga kufunga CCTV kwenye eneo la kunyolea, reception na sehemu nyingine muhimu kwa ajili ya usalama na ufuatiliaji wa biashara. Isipokuwa ndani ya chumba cha scrub, ambapo sitaweka kamera kwa sababu za faragha.
Sasa naomba ushauri wa wenye uzoefu wa biashara hii. Je, mfumo gani ni bora zaidi wa usimamizi? Niwaajiri vinyozi kwa mshahara wa mwezi, au nimkabidhi kinyozi mmoja asimamie saluni? Au kila kinyozi awe na kiti chake na anikabidhi makubaliano ya mapato kila wiki au kila siku? Pia nimekuwa nikifikiria kama ni vyema kuajiri receptionist au secretary ambaye kazi yake iwe kupokea wateja, kurekodi mauzo, kukusanya mapato na kusimamia hesabu, kisha vinyozi walipwe kwa wiki au mwisho wa mwezi. Sipendi mfumo wa kuwalipa kwa siku.
Kwa wenye uzoefu, hasa wa biashara za barber shop katika maeneo yenye shughuli nyingi kama Morogoro, mnanishauri mfumo gani wa malipo na usimamizi? Kama ni mshahara wa mwezi, kwa sasa ni kiwango gani kinachofaa kwa kinyozi mzuri? Na kama ni mfumo wa makabidhiano ya mapato, kwa kawaida kila kinyozi anatakiwa kukabidhi kiasi gani kwa wiki ili biashara iwe na faida kwa pande zote?
Karibuni sana kwa ushauri, uzoefu na maoni yenu. Asanteni.