Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

We wapangie tu kwa siku wakabidhi kila mtu kiasi flani haijalishi wamenyoa vichwa vingapi.

Ukipanga kiasi cha hela kwa kichwa watakudanganya. Kufuatilia masaa yote kwa CCTV ni ngumu!
CCTV ina option ya playback mkuu, na unaweza uka play kwa speed ya haraka so matukio ya siku nzima naweza yatazama ndani ya nusu saa na kuhesabu kila kichwa.
 
Huyu unaemuweka akizoea. Yeye ndio atakuwa anakupiga. Au anaungana na vinyozi wanakuwa hawaandiki kwenye kitabu.

Kinyozi kwa wiki akisema biashara mbaya . Bas unampa siku 1 afidie deni lako. Na wiki hiyo akishindwa . Unamtoa . Unatafuta kinyozi mwingne.

Ukiwa lelemama na mpole mpole watakupanda kichwan.
Itakua n rahisi kumbana maana kama kwa makadirio mapato ni elfu 40 kwa siku akianza stori za elfu 26 unamlipa chake anasepa unaajiri mwingine fasta hapo lazima kutakua na nidhamu ya kazi.. lazima uwe mkali ili kazi iende
 
Ni uhuni tu! Wanataka tulipe 10,000/- ya "miundombinu ya saluni ya kike au kiume" ukiisoma hiyo sheria yao wame-define hiyo miundombinu kama ifuatavyo:-
"eneo la wazi, jengo au sehemu nyingine yoyote inayotumika kufanyia kazi za sanaa kwa madhumuni ya burudani, sherehe, urembo, ulimbwende na utanashati."

Huu utaratibu ni mpya hiyo kanuni imeanza kitumika julai 2025.
Mmmh sikujua kabla!
Asante kwa kunijuza.
 
Achana na Hesabu.
Hesabu mwambie Kila Kinyoz akutumie 150k au 200k kila wiki, atume mwenyewe.

Chagua kinyozi mmoja ndio awe msimamizi wa Saloon, na ndio hii yeye atahakikisha vipodozi viko na vikiisha vinanunuliwa na wao wenyewe.

Ww unatakiwa kununua kwa mara ya kwanza. Baada ya hapo. Haununui ww. Wananunua Vinyozi.

Ni Kama ilivyo Magic shaving powder au spirit, au tissue na vile vidude vya kufunga kabla ya kuwekewa kitambaa.

Hivi ukivinunua wakat unafungua Saloon. Vikiisha haununui ww tena.

Kila wiki unaenda kukagua saloon yako. Na ww mahitaj yanayokuhusu ni Maji na umeme.

Sabuni, na vitu kama hivyo ni wao wanahusika na kununua. Wakiongozwa na kiongozi wao.
Ww ni kwenda kwa kushtukiza kukagua mazingira ya saloon yako na kama.vitu viko.

Pia Wadada wa Saloon usiwazoee kabisa. Yaan wale hawakuhusu. Wala usiwatafute ww. Vinyozi huwa wana connevction zao na watajua watawatoa wapi. Na hata kulipana watajua wenyewe. Na Usije ukawatoomb* wakasambaza maneno ukajiharibia Heshima yako 😊😊😊😊
Mkuu umetema nondo sana
 
Back
Top Bottom