Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

Huku niliko chakula na mahali pa kulala ndio vitu vyenye gharama!, ni machimboni, Chumba cha chini ni 50k , ugali dagaa 2000!

Kumiliki ghetto ni mahari tosha kwa mtoto wa kike. Kyuuuma ni bei rahisi kuliko chakula!
wapi huko kakaaa
 
Asante kwa ushauri wako ila usifikiri kila biashara unayoiona basi mmiliki ndio msimamizi.

Bakhresa ana biashara kibao unafikiri anazisimamia mwenyewe au kaweka wasimamizi na kubaki mmiliki? Ni namna unavyoweka mikakati na "systems" ndiyo husababisha biashara kufanikiwa.

Ukiona unaendesha biashara ambayo ukikosekana mwezi mmoja haiwezi kujiendesha basi ujue bado una safari ndefu. Na biashara nyingi za kiafrika ndio zipo hivyo ndo maana mmiliki akiumwa au kufa na biashara inakufa naye.
Mkuu punguza kuwasikiliza motivation speakers ambayo biashara yao ni kukuuzia matumaini. Huu ni wakati wako wa kufanya kazi zote hapo kwenye ofisi yako kwa sababu biashara yako ni changa inayoanza. Hata kina Bill Gates na Mark Zuckerberg walikuwa wanaandika codes wenyewe wakati wanaanzisha biashara za na baadae ndo wakaajiri magenius. Hadi biashara inajiendesha lazima wewe mmiliki uwe umepambana sana kufikia hiyo hatua.
 
Usikariri maisha mkuu! Sio kila biashara inafanyika hivyo.

Mimi nina run AirBnB property, na tangu ni design layout ya nyumba na kuweka furniture na inventory na ku list property kwenye AirBnB website, sijawahi kuwepo kwenye property kupokea mteja, kusupply inventory au guest requests! Niliweka msimamizi na kila kitu kinaenda.

Mteja akibook ninapata notification kwa app, na yule msimamizi anapokea booking na ku confirm na kuendelea na process zote. Mimi huwa napita tu kila baada ya wiki mbili au mwezi kucheki inventory na kulipa bill za maji na umeme.
 
Kuna mtu nimemfuata nimempiga maswali mazito uyu ni mmiliki wa barbershop flan apa idodomya pia ni kinyoz mstaafu,majibu yake yapo kitaalamu sana hasa jinsi ya kusimamia ofisi,kukusanya pato,na kulipa wafanyakaz na majibu yake juu ya swali lako ni kua yeye amemuajir kinyoz mmoja tu kati ya vinyoz sita(6)waliopo apo na yeye huchukua 350k kwa wiki umeme,vipodoz,pesa ya usafi na kulipana na wahudumu wengine hayamuhusu,yeye analipa maji,pango la ofisi,tra na wi-fi tu na kwa wiki anatembelea x2 au 1 na amefanya hivyo kutokana na uzoefu kama kinyoz
 
Vinyoz na wadada wa scrub hawalipwi hao ni kama mabaa medi wanajilipa wenyewe kumbuka hawa ndio ofis zenyewe na wateja huwafuata hawa na kumbuka kua hawa watu kila siku lazima waondoke na pesa yamatumizi yao,usafir na posho
 
Kuna mtu nimemfuata nimempiga maswali mazito uyu ni mmiliki wa barbershop flan apa idodomya pia ni kinyoz mstaafu,majibu yake yapo kitaalamu sana hasa jinsi ya kusimamia ofisi,kukusanya pato,na kulipa wafanyakaz na majibu yake juu ya swali lako ni kua yeye amemuajir kinyoz mmoja tu kati ya vinyoz sita(6)waliopo apo na yeye huchukua 350k kwa wiki umeme,vipodoz,pesa ya usafi na kulipana na wahudumu wengine hayamuhusu,yeye analipa maji,pango la ofisi,tra na wi-fi tu na kwa wiki anatembelea x2 au 1 na amefanya hivyo kutokana na uzoefu kama kinyoz
Ni hesabu fair japo kwa jicho la kibiashara naona kuna leakage ya pesa nyingi ukizingatia idadi ya vinyozi.
 
Hapo njia rahisi ni kuajiri mtu wa kupokea hela sio kila mtu apokee hela.

Hivo itakua rahisi kusolve tatizo la wizi cha kisingizio kua biashara n mbaya mtu akianza wizi unamfukuza na kuajiri mwingine chapu...

Hii ndo njia nayotumia mimi kwenye haso zangu
 
Naichukua hii
 
Ushauri wangu kama mtu niliyechangia mageuzi ya uwepo wa Barbershop Bora Kwa Dar(Kisarano iliyokuwa Tabata shule) baada ya kuangalia mapungufu ya zilizokuwa saloon tajwa wakati huo ya Bitebo na nyingine maeneo ya Masaki na Sinza.

Kwanza weka Hesabu Kwa kila kinyozi unayemkabidhi kiti.

Wape mtaji wa Vitendea Kazi kama Black,magic na masaga zaga mengine,kama Crub za aina zote,Mask za aina zote na hata visafisha miguu

Kwamba huo ni mtaji wanapaswa kuulinda na kukukabidhi siku watakayoacha Kazi.

Jukumu la Mashine za kunyolea na Umeme ni lako.

Weka Madada wa kusaidia Kazi hizo ambao utawalipa wewe na weka msimamizi wa Kazi (ofisi hiyo) ikiwa na misingi yote ya ajira.

Kisha Kila wiki Kila kiti kikukabidhi Hesabu mliyokubaliana kabla ya kuanza Jumatatu ya wiki mpya

Sikiliza wateja wako na Fanya maboresho ya mara Kwa mara(Mtafute king Azizi huyu ana Saloon maeneo ya Masaki na Mbezi Kwa Ushauri) sema mpigaji Sana

Mada
 
Asante sana
 
yeye amemuajir kinyoz mmoja tu kati ya vinyoz sita(6)waliopo apo na yeye huchukua 350k kwa wiki umeme,vipodoz,pesa ya usafi na kulipana na wahudumu wengine hayamuhusu,yeye analipa maji,pango la ofisi,tra na wi-fi tu na kwa wiki anatembelea x2 au 1 na amefanya hivyo kutokana na uzoefu kama kinyoz

Na huu ndio mfumo mzuri.
Hata kama hao wote sita angewaajiri. Wote wangekuwa wanatuma hesabu separate. Kila wiki.

Na hayo mengne yanakuwa kama ulivyosema.
 
Hapo njia rahisi ni kuajiri mtu wa kupokea hela sio kila mtu apokee hela.

Hivo itakua rahisi kusolve tatizo la wizi cha kisingizio kua biashara n mbaya mtu akianza wizi unamfukuza na kuajiri mwingine chapu...

Hii ndo njia nayotumia mimi kwenye haso zangu
Huyu unaemuweka akizoea. Yeye ndio atakuwa anakupiga. Au anaungana na vinyozi wanakuwa hawaandiki kwenye kitabu.

Kinyozi kwa wiki akisema biashara mbaya . Bas unampa siku 1 afidie deni lako. Na wiki hiyo akishindwa . Unamtoa . Unatafuta kinyozi mwingne.

Ukiwa lelemama na mpole mpole watakupanda kichwan.
 
Mimi sitakwepo hapo muda wote japo CCTV zitakwepo, hii kuwalipa kwa siku iwe flat rate au kwa idadi ya vichwa alivyonyoa kinyozi?
We wapangie tu kwa siku wakabidhi kila mtu kiasi flani haijalishi wamenyoa vichwa vingapi.

Ukipanga kiasi cha hela kwa kichwa watakudanganya. Kufuatilia masaa yote kwa CCTV ni ngumu!
 
Habari zenu wakuu? Natumaini wote mpo salama na mnaendelea vizuri.

Nina mtaji ambao ninatarajia kuwekeza katika kufungua barber shop eneo la Msamvu, karibu na Stendi Kuu ya Morogoro. Mpango wangu ni kuwa na viti vinne vya kisasa vya kunyolea, pamoja na chumba maalumu cha scrub chenye vitanda viwili na sinki la kuoshea. Tayari nimefanya makadirio ya gharama zote zinazohitajika, ikiwemo AC, heater ya maji, partition za ndani, pamoja na kupata eneo la biashara.

Niliwahi kumiliki salon ndogo miaka iliyopita, lakini niliiuza kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Mimi si kinyozi, hivyo nilishindwa kuisimamia ipasavyo. Safari hii nimejipanga vizuri zaidi. Pia nimepanga kufunga CCTV kwenye eneo la kunyolea, reception na sehemu nyingine muhimu kwa ajili ya usalama na ufuatiliaji wa biashara. Isipokuwa ndani ya chumba cha scrub, ambapo sitaweka kamera kwa sababu za faragha.

Sasa naomba ushauri wa wenye uzoefu wa biashara hii. Je, mfumo gani ni bora zaidi wa usimamizi? Niwaajiri vinyozi kwa mshahara wa mwezi, au nimkabidhi kinyozi mmoja asimamie saluni? Au kila kinyozi awe na kiti chake na anikabidhi makubaliano ya mapato kila wiki au kila siku? Pia nimekuwa nikifikiria kama ni vyema kuajiri receptionist au secretary ambaye kazi yake iwe kupokea wateja, kurekodi mauzo, kukusanya mapato na kusimamia hesabu, kisha vinyozi walipwe kwa wiki au mwisho wa mwezi. Sipendi mfumo wa kuwalipa kwa siku.

Kwa wenye uzoefu, hasa wa biashara za barber shop katika maeneo yenye shughuli nyingi kama Morogoro, mnanishauri mfumo gani wa malipo na usimamizi? Kama ni mshahara wa mwezi, kwa sasa ni kiwango gani kinachofaa kwa kinyozi mzuri? Na kama ni mfumo wa makabidhiano ya mapato, kwa kawaida kila kinyozi anatakiwa kukabidhi kiasi gani kwa wiki ili biashara iwe na faida kwa pande zote?

Karibuni sana kwa ushauri, uzoefu na maoni yenu. Asanteni.
As for me, baba yang anayo saloon na njia anayopata mapato ni very simple, anakabizi saloon kw vinyoz then kila kiti mapato kwa siku elfu 8 tu, na ipo zanzibar , kuna viti vinne.. hajaweka cctv wala nn na ikitokea kinyoz kazingua kwa siku 3 mfululizo bas anazinguana nae .. very simple
Habari zenu wakuu? Natumaini wote mpo salama na mnaendelea vizuri.

Nina mtaji ambao ninatarajia kuwekeza katika kufungua barber shop eneo la Msamvu, karibu na Stendi Kuu ya Morogoro. Mpango wangu ni kuwa na viti vinne vya kisasa vya kunyolea, pamoja na chumba maalumu cha scrub chenye vitanda viwili na sinki la kuoshea. Tayari nimefanya makadirio ya gharama zote zinazohitajika, ikiwemo AC, heater ya maji, partition za ndani, pamoja na kupata eneo la biashara.

Niliwahi kumiliki salon ndogo miaka iliyopita, lakini niliiuza kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Mimi si kinyozi, hivyo nilishindwa kuisimamia ipasavyo. Safari hii nimejipanga vizuri zaidi. Pia nimepanga kufunga CCTV kwenye eneo la kunyolea, reception na sehemu nyingine muhimu kwa ajili ya usalama na ufuatiliaji wa biashara. Isipokuwa ndani ya chumba cha scrub, ambapo sitaweka kamera kwa sababu za faragha.

Sasa naomba ushauri wa wenye uzoefu wa biashara hii. Je, mfumo gani ni bora zaidi wa usimamizi? Niwaajiri vinyozi kwa mshahara wa mwezi, au nimkabidhi kinyozi mmoja asimamie saluni? Au kila kinyozi awe na kiti chake na anikabidhi makubaliano ya mapato kila wiki au kila siku? Pia nimekuwa nikifikiria kama ni vyema kuajiri receptionist au secretary ambaye kazi yake iwe kupokea wateja, kurekodi mauzo, kukusanya mapato na kusimamia hesabu, kisha vinyozi walipwe kwa wiki au mwisho wa mwezi. Sipendi mfumo wa kuwalipa kwa siku.

Kwa wenye uzoefu, hasa wa biashara za barber shop katika maeneo yenye shughuli nyingi kama Morogoro, mnanishauri mfumo gani wa malipo na usimamizi? Kama ni mshahara wa mwezi, kwa sasa ni kiwango gani kinachofaa kwa kinyozi mzuri? Na kama ni mfumo wa makabidhiano ya mapato, kwa kawaida kila kinyozi anatakiwa kukabidhi kiasi gani kwa wiki ili biashara iwe na faida kwa pande zote?

Karibuni sana kwa ushauri, uzoefu na maoni yenu. Asanteni.
Na mzee anakuw majukum yake ni matengenez ya duka na leseni lkn vilivobaki ni juu yao vinyoz, hata ikitokea kwa siku kaingiza elf 50 ,just ww akupe elfu 8 tu na hata kama kwa siku kaingiza elfu 8 ajue kama elfu 8 ipo ya boss au siku kama hio atleast akupe elfu 7
 
Huyu unaemuweka akizoea. Yeye ndio atakuwa anakupiga. Au anaungana na vinyozi wanakuwa hawaandiki kwenye kitabu.

Kinyozi kwa wiki akisema biashara mbaya . Bas unampa siku 1 afidie deni lako. Na wiki hiyo akishindwa . Unamtoa . Unatafuta kinyozi mwingne.

Ukiwa lelemama na mpole mpole watakupanda kichwan.
Imekaa vizuri hii strategy japo kutakuwa na cctv cameras kila angle potential, sasa sijui watasingiziaje biashara mbaya wakati mm nikicheki cctv recordings naona watu kadhaa walikuja wakanyolewa.
 
BASATA unalipa fee ya nini? Ebu nijuze mkuu
Ni uhuni tu! Wanataka tulipe 10,000/- ya "miundombinu ya saluni ya kike au kiume" ukiisoma hiyo sheria yao wame-define hiyo miundombinu kama ifuatavyo:-
"eneo la wazi, jengo au sehemu nyingine yoyote inayotumika kufanyia kazi za sanaa kwa madhumuni ya burudani, sherehe, urembo, ulimbwende na utanashati."

Huu utaratibu ni mpya hiyo kanuni imeanza kutumika julai 2025.
 
Back
Top Bottom