Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

Ninafungua Barbershop: Je Vinyozi Walipwe Mishahara au Wakabidhi Hesabu?

Mfumo bora zaidi duniani kote wa saluni ni commission, mfano 40% kwa kinyozi na 60% kwako baada ya kutoa gharama za umeme na vitu vingine au mnawekeana 50/50 kama vifaa vingine vidogo vidogo wanajitegemea wao wenyewe. Hii itamfanya kinyozi ajue kuwa asipofanya kazi na yeye hatoishi vizuri mjini na akijituma anapata hela, ni njia nzuri kwa mtazamo wangu.
 
Fanya kama saloon za kike, walipe per day, weka cashier, na hakikisha unaweka mfumo mzuri wa rekodi,kila mteja arekodiwe kwenye mfumo (QMS)
Itakusaidia kujua umehudumia wateja wangapi, huduma ipi inatoka zaidi,nani anafanya kazi kati ya vinyozi wako wote n.k
Asante, hii nimeipenda! Na kuwalipa je? Walipwe flat rate au per performance?
 
Habari zenu wakuu? Natumaini wote mpo salama na mnaendelea vizuri.

Nina mtaji ambao ninatarajia kuwekeza katika kufungua barber shop eneo la Msamvu, karibu na Stendi Kuu ya Morogoro. Mpango wangu ni kuwa na viti vinne vya kisasa vya kunyolea, pamoja na chumba maalumu cha scrub chenye vitanda viwili na sinki la kuoshea. Tayari nimefanya makadirio ya gharama zote zinazohitajika, ikiwemo AC, heater ya maji, partition za ndani, pamoja na kupata eneo la biashara.

Niliwahi kumiliki salon ndogo miaka iliyopita, lakini niliiuza kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Mimi si kinyozi, hivyo nilishindwa kuisimamia ipasavyo. Safari hii nimejipanga vizuri zaidi. Pia nimepanga kufunga CCTV kwenye eneo la kunyolea, reception na sehemu nyingine muhimu kwa ajili ya usalama na ufuatiliaji wa biashara. Isipokuwa ndani ya chumba cha scrub, ambapo sitaweka kamera kwa sababu za faragha.

Sasa naomba ushauri wa wenye uzoefu wa biashara hii. Je, mfumo gani ni bora zaidi wa usimamizi? Niwaajiri vinyozi kwa mshahara wa mwezi, au nimkabidhi kinyozi mmoja asimamie saluni? Au kila kinyozi awe na kiti chake na anikabidhi makubaliano ya mapato kila wiki au kila siku? Pia nimekuwa nikifikiria kama ni vyema kuajiri receptionist au secretary ambaye kazi yake iwe kupokea wateja, kurekodi mauzo, kukusanya mapato na kusimamia hesabu, kisha vinyozi walipwe kwa wiki au mwisho wa mwezi. Sipendi mfumo wa kuwalipa kwa siku.

Kwa wenye uzoefu, hasa wa biashara za barber shop katika maeneo yenye shughuli nyingi kama Morogoro, mnanishauri mfumo gani wa malipo na usimamizi? Kama ni mshahara wa mwezi, kwa sasa ni kiwango gani kinachofaa kwa kinyozi mzuri? Na kama ni mfumo wa makabidhiano ya mapato, kwa kawaida kila kinyozi anatakiwa kukabidhi kiasi gani kwa wiki ili biashara iwe na faida kwa pande zote?

Karibuni sana kwa ushauri, uzoefu na maoni yenu. Asanteni.
Hongera kijana
 
Mimi sitakwepo hapo muda wote japo CCTV zitakwepo, hii kuwalipa kwa siku iwe flat rate au kwa idadi ya vichwa alivyonyoa kinyozi?

System nzur ni wao uwape hesabu na kukulipa kwa wiki.

Chagua msimamizi ila usifanye yeye ndio akusanye hela. Hela kila kinyozj akutumie ww Direct. Kila wiki.
Kiongozi Yeye asimamie Umeme, usafi, maji na manunuz ya vitu vinavyotumika.

Kila kinyoz ataelewana na kumlipa mdada kama akimuosha na kumfanyia huduma mteja wake.

Vinyoz wanafanya biashara nying weekend. Kwahiyo kuwawekea flat rate Watanungunika. Maana weekdays hawawez pata hela mingi.
 
Mfumo bora zaidi duniani kote wa saluni ni commission, mfano 40% kwa kinyozi na 60% kwako baada ya kutoa gharama za umeme na vitu vingine au mnawekeana 50/50 kama vifaa vingine vidogo vidogo wanajitegemea wao wenyewe. Hii itamfanya kinyozi ajue kuwa asipofanya kazi na yeye hatoishi vizuri mjini na akijituma anapata hela, ni njia nzuri kwa mtazamo wangu.
Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.
 
Kila kinyoz ataelewana na kumlipa mdada kama akimuosha na kumfanyia huduma mteja wake.
Hapa kwa kila kinyozi kuelewana na kumlipa mdada fafanua zaidi maana ninaweka cosmetics kibao kwa ajili ya scrub na facial, steaming etc na scrub zipo za bei tofauti from 5K, 10K mpaka 30K per person.

Haya mapato ya huku nitaya-onitor vipi bila leakage? Plus inasemekana kwenye barbershop pesa mingi ipo kwenye hizi huduma za scrub,facial etc.
 
Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.
Ukisema 50/50 Ndio mfumo mzuri kwa sasa ndugu, hapo ww ni kulipa kodi tu. Bill ya umeme, maji na vipodozi ni juu yao. Kwa upande wa kwenye scrub kule manicure na pedicure vipodozi vya kwako na wao hawapati mgao wowote.
 
Asante kwa ushauri wako lakini 50/50 percent HAPANA! Naweka mtaji (10 M+), nalipia rent, nalipia leseni, nalipa fee BASATA, nalipa kodi TRA, bill za maji, umeme. 50/50 HAPANA kabisa.
Haujanielewa vizuri naona, maana yangu ni kwamba kila mwisho wa wiki au mwezi, mnakuwa mnapiga hesabu. Mfano, saluni imeingiza milioni mbili, unakata kwanza gharama zako zote za mwezi huo mfano makadirio ya umeme, maji, kodi, na uchaji wa leseni/BASATA/TRA). Ile net profit inayobaki ndio mnaigawa kwa asilimia mlizokubaliana mfano wewe 60% au 70%, vinyozi 30% au 40%.
 
Hapa nimekuelewa....Huku kwenye scrub nita-monitor vipi mapato? Maana sitokwepo hapo muda wote.
Ukisema 50/50 Ndio mfumo mzuri kwa sasa ndugu, hapo ww ni kulipa kodi tu. Bill ya umeme, maji na vipodozi ni juu yao. Kwa upande wa kwenye scrub kule manicure na pedicure vipodozi vya kwako na wao hawapati mgao wowote.
 
Haujanielewa vizuri naona, maana yangu ni kwamba kila mwisho wa wiki au mwezi, mnakuwa mnapiga hesabu. Mfano, saluni imeingiza milioni mbili, unakata kwanza gharama zako zote za mwezi huo mfano makadirio ya umeme, maji, kodi, na uchaji wa leseni/BASATA/TRA). Ile net profit inayobaki ndio mnaigawa kwa asilimia mlizokubaliana mfano wewe 60% au 70%, vinyozi 30% au 40%).
Ubarikiwe!
 
Hapa nimekuelewa....Huku kwenye scrub nita-monitor vipi mapato? Maana sitokwepo hapo muda wote.
Kutokuwepo sio ishu funga cctv then tafuta mdada anaeweza kuaminika , siku moja moja unatuma hata watu wakafanye huduma alafu na kiasi watakachotoa then we pitia daftari uone kama kimeandikwa kilichotolewa hapo hata wao wenyew wataogopa kwamba unafatilia
 
Back
Top Bottom