Ninafuraha sana gari imepona

SaaMbovu

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
6,027
Reaction score
5,344
Habari.

Napenda kushare uzoefu hapa kidogo nina gari ndogo ambayo ni VOLTZ na nimekuwa nayo sasa kwa takriban 3 years. Miezi kama 10 iliyopita nilianza kuona gari inakosa nguvu kwa mbali. Baadae nikawa naona maybe gari yangu ndivyo ilivyo. Kadiri siku zikivyozidi kwenda mbele gari ikazidi kukosa nguvu nikafikia hatua mlima siwezi kupanda na nikipanda ni kwa tabu sana.

Baadhi ya mafundi wakaniambia ni Transmission fluid ibadilishwe na baada ya kubadikisha bado tatizo likawa palepale. Nikaenda kwa mwingine akasema hapa tatizo ni transmission fluid filter ni chafu isafishwe baada ya kufanya hivyo tatizo likawa bado. Fundi mwingine akaniambia tatizo ni plugs maana tangu ninunue plugs sijawahi badilisha.

Baada ya kubadili tatizo likawa palepale. Sasa jana nikapeleka sehemu ambayo wanabei kidogo gari ilifanyiwa diagnosis na kugundua kwamba tatizo likikuwa kwenye pump na fuel return valve. Baada ya kurekebishwa gari imekuwa na nguvu kuliko hata nilivyoinunua.

Kiukweli nina furaha sana maana nilikuwa nawaza kuiuza na sasa nimefuta wazo hilo maana ningeuza ningepata hasara kubwa sana.

Karibuni.
 
Wengi wa mafundi bongo wapiga ramli tu..ukiwa serious peleka gari yako centres zenye akili
Ni kweli. Maana mpaka napeleka hapo tayari nikishatumia almost Tsh. 200k na tatizo lilikuwa bado.
 
Ungemaliza basi japo haka ka week kuja kuonesha furaha yako humu maana sio baada ya siku tatu unaanza mayowe alitokea mteja bora ningeuza.
 
Kadiri technology inavyozidi mbele itafika kipindi hawa mafundi wetu wa mtaani watapotea kama vile TV za chogo
Ni kwel kaka, mi mwenyewe nimeshashuhudia sana watu wakinunulishwa spare parts kumbe tatizo nilingine kabisa, kiufupi huwa kaz kwa kuhic hic tu, mi mwenyewe nina toyota allex nikiwasha inatoa kelele fulani hv kama ya kunok halafu inaacha bac nimehangaika mpaka bass kila funɗ anakuambia nunua hiki lakin hakuna kitu.
 
Peleka Kwenye diagnosis mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…