Ninafuraha sana gari imepona

Ninafuraha sana gari imepona

Habari.

Napenda kushare uzoefu hapa kidogo nina gari ndogo ambayo ni VOLTZ na nimekuwa nayo sasa kwa takriban 3 years. Miezi kama 10 iliyopita nilianza kuona gari inakosa nguvu kwa mbali. Baadae nikawa naona maybe gari yangu ndivyo ilivyo. Kadiri siku zikivyozidi kwenda mbele gari ikazidi kukosa nguvu nikafikia hatua mlima siwezi kupanda na nikipanda ni kwa tabu sana.

Baadhi ya mafundi wakaniambia ni Transmission fluid ibadilishwe na baada ya kubadikisha bado tatizo likawa palepale. Nikaenda kwa mwingine akasema hapa tatizo ni transmission fluid filter ni chafu isafishwe baada ya kufanya hivyo tatizo likawa bado. Fundi mwingine akaniambia tatizo ni plugs maana tangu ninunue plugs sijawahi badilisha.

Baada ya kubadili tatizo likawa palepale. Sasa jana nikapeleka sehemu ambayo wanabei kidogo gari ilifanyiwa diagnosis na kugundua kwamba tatizo likikuwa kwenye pump na fuel return valve. Baada ya kurekebishwa gari imekuwa na nguvu kuliko hata nilivyoinunua.

Kiukweli nina furaha sana maana nilikuwa nawaza kuiuza na sasa nimefuta wazo hilo maana ningeuza ningepata hasara kubwa sana.

Karibuni.
Ni wapi huko mkuu na bill yao ikoje mkuu. Msaada katika hilo
 
Likiwa bovu ndio unauza mkuu? Ulitaka 'kumshikisha' mtu?
Hii ni tabia mbaya kabisa, Mwenyezi MUNGU aniepushe nayo. Kumuuzia mtu kitu kibovu na wakati unajua haifai kabisa
 
Ni kwel kaka, mi mwenyewe nimeshashuhudia sana watu wakinunulishwa spare parts kumbe tatizo nilingine kabisa, kiufupi huwa kaz kwa kuhic hic tu, mi mwenyewe nina toyota allex nikiwasha inatoa kelele fulani hv kama ya kunok halafu inaacha bac nimehangaika mpaka bass kila funɗ anakuambia nunua hiki lakin hakuna kitu.
Wakati mwingine bora kukubali gharama. Peleka kwenye centre za toyota mkuu
 
Ungemaliza basi japo haka ka week kuja kuonesha furaha yako humu maana sio baada ya siku tatu unaanza mayowe alitokea mteja bora ningeuza.
Huu sasa ni mwezi wa 4 bado wiki moja tangu kutoa uzi huu. Gari bado ipo vizuri sana.
Pia nilipiga safari zifuatazo.
1. Mwanza Arusha via Singida.
2. Arusha Dodoma via Kondoa
3. Dodoma Dar es Salaam
4. Dar Morogoro then back to Dar
5. Dar Babati via Dodoma and Kondoa
6. Babati Mwanza via Singida.

Hiyo nadhani ni feedback nzuri.
 
Back
Top Bottom