Ninafuraha sana gari imepona

Peleka kwa wataalam hilo lutaisha tu. Vip walisha angalia mfumo wa starter maana hiyo kazi yake ni kuwasha gari na kutoka inabaki off.
Walishaangalia kaka....ila inavyoonesha ni kama oili inachelewa kupanda kwa haraka pindi ninapo washa gari tu, inaonekana kama kuna kifilter hakipitishi oil chap ila wanashindwa kukibain kikowapi, maana inapigia kelele kwenye kem shafty
 
Mkuu ukumbuke na sheria za barabara kwa ajili ya usalama wako na watumiaji wengine wa barabara.
 

Hivi gari ya petrol inatumia pump? Naulizatu.
 
Engine computer diagnosis ndio habari ya mjini kwa sasa,ila kama unapendelea ile ya kujaribu hiki acha kile lazima utaliwa sana...
 
Nilinunua taa kubwa moja ya mbele kwa milioni moja na laki mbili nilichoka kabisa.
Mie waliiba fog light 1 niliipata kwa 80k.
But wauzaji wengi walikuwa wanataka 150k
 
Kwenda kwa mafundi wa mtaani ni sawa kwenda kwa waganga wa kienyeji
 
Kaka hiiyo itakuwa ni fly wheel yangu ilikuwa na tatizo hilo hilo kapona.
 
Kaka hiiyo itakuwa ni fly wheel yangu ilikuwa na tatizo hilo hilo kapona.
Naomba unipe mchanganuo kidogo kaka, ulifanyaje hadi likaishaaa....maana mwenzio nilishusha hadi injin nikaweka nyingine ila tatizo lilirudia pale pale baada ya cku chache, nilichoka kabisa na kujisemea kumbe nilibadili injini bure tu broo....mpaka sasa bado cjui la kufanya kaka.
 
Ingia google andika fly wheel problem itakuletea,mafundi siku hizi ni wa kuelekeza,fundi wangu nilimwelekeza alipofungua tu fly wheel na kuifunga tena gari ilitulia ajabu. Hiyo sio injin ni fly wheel labda imekatika au nati zimelegea.Fanya hivyo mkuu utaleta mrejesho hapa.
 
Pamoja sana mkuu
 
Fuel pump uliweka mpya au walifanyaje mkuu?
 
Kama hilo tatizo bado lipo...fanya hivi..
Kama unatumia Engine oil SAE 40 imwage na uweke 5w30....endapo tatizo litaendelea itakuwa ni major issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…