Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Katika makampuni hovyo hapa nchini ni Benki za hapa, TIGO nao ni wahuni sana na wafanyakazi wake wanashirikiana na Matapeli kutapeli wateja.
 
Majizi kabisa hya CRDB,wanaamua tu kujikatia hela bila kuwajulisha wateja.
 
njoo nmb kidogo wana nafuu naweza kutoa mfno 500k nkakatwa mpka buku 2 tu kwenye ATM

kingine nachopendea ni ukiwa na app yao kucheki balance ni bure bas nikiwa na vijisent vyangu kila nikitoa hela lazma nihakiki mzigo wangu to be honest kwa hilo naenjoi nao
Daaah sikutegemea kabisa
 
naona crdb inaongoza kwa malalamiko ngoja niwaangalie kwa miezi 3 nawahama wakinizingua
 
Nategemea kipindi hiki cha ukosefu wa ajira vijana waliotoka law school watanusa kitu😊😊
Bongo hakuna Law School, bali kuna Low School tu!
Tungekua na Law School mbona huduma mbalimbali nchini zingenyooka kwa jinsi vile wangekua wananyooka na watoa huduma.
 
Mshahara unakatwa PAYE
Alafu ukenda benki kuchukua unakatwa tozo na VAT
Mshahara mmoja unakaatwa mara tatu !!
Ukiweka hakuna tozo ukichukua kuna tozo ZA NINI
 
Mabank ya Kitanzania sijui yanafanyaje biashara yani makato ni makubwa kama una ka hela ka ngama ni bora uweke chini ya godoro tu.

Ndiomaana yanapata super profit kila msimu.
Ukitoka nje ya nchi ukafanikiwa kutumia Banks za wenzetu ndio utajua Banks za Bongo ni Wanyonyaji wasio na huruma kama enzi za ukoloni.

We ulishaona wapi kuangali salio online kwenye App eti napo unakatwa?

Wenzetu miamala yote ni bure, unalipia card fee tu kwa mwezi. Tena pesa ndogo kweli.
 
Banks za wenzetu wanapata faida kutokana na riba za mikopo. Sio kuwanyonya watu maskini kwa kuwawekea makato kila wanapofanya miamala. Eti kuangalia salio la pesa zako napo mpaka ukatwe. Huu ni unyonyaji ulio kubuhu!
 
Badae utasikia wanajipongeza kwa kupata faida kubwa. Faida kubwa za kuwaibia watu fukara. Hawa watu Mungu anawaona!
 
Ukitoka nje ya nchi ukafanikiwa kutumia Banks za wenzetu ndio utajua Banks za Bongo ni Wanyonyaji wasio na huruma kama enzi za ukoloni.

We ulishaona wapi kuangali salio online kwenye App eti napo unakatwa?

Wenzetu miamala yote ni bure, unalipia card fee tu kwa mwezi. Tena pesa ndogo kweli.
Hahaa bongo ni balaa mkuu.
Nje sijawahi toka ila bongo makato ni tatizo

Majuzi nilienda exim bank nina account huko sasa nikataka huduma ya kuangalia balance kwenye simu mana hiyo account ninaitumia kwa biashara so niangalie mtu akisema ka transfer hela au cheque ime clear.

Bwana wee nikapewa menu namba niweze kujiunga ile * ngapi ngapi sijui# nikaona inakataa sasa nikauliza why inakataa nikaambiwa lazima uwe n hela kwenye simu yako(sio kifurushi ni hela mana kifurushi kilikuwepo)

Yani kuangalia balance ukatwe na mtandao wa simu na kisha bank yako ikukate tena. Nikawaambia nitarudi baadae.
 
Hahahaaa!! Mpk leo bado huja sepa? Wala hawatajua kua umeama. Ila watahisi umefaliki dunia tu.
 
Back
Top Bottom