Zinafanana kama vituo vya mafuta, Tanzania hakuna ubunifu hakuna ushindani yaani ukienda Bank moja wakikupa jibu basi wala usihangaike kwenda Bank nyingine ukadhani utapata jibu au huduma tofauti wafanya kazi kwa kukariri tu huduma za wateja ni walewale hawana jipya. mbaya zaidi bank yenye wateja wengi na yenye wateja wachache ni wale wale hakuna ushindani wa ubunifu unategemea mdogo akaja kivingine ile we mkubwa kuvuta watu ila narudi pale pale hawana jipya wala ubunifu. Wakati mmoja nilidafiri mji mmoja nikafikia Hotel moja nzuri sana tu japo mji ule una Hotel nyingi tu 5 star zinafanana kwa ubora ila hii Hotel kufika pale hujazi chochote unapewa chumba then anakuja yule mtu wa reception na Laptop yake kwa adabu anakuja room anafanya taratibu zote chumbani inakufanya usiwasahu sababu wanakufanya ujisikie Bill gates kumbe huna lolote kubwa huu ni ubunifu kuwa tofauti na wengine. Ila Tz Bank zote sawa kampuni zote za simu sawa tofauti majina ya ajabu tu ya package zao. Utakuwa Bank inajitangaza sana sasa mteja fika Bank hao customer care utatapika wakati walitakiwa wafanye juhudi wakunase usitoke ili ukienda nje uwatangaze kwa mazuri ndio strategy ya kujitangaza ila ukitoka hapo hata kuangalia nyuma huangalii jioni unawaona kwenye TV Bank bora fika tawi lolote bla bla bla ujinga mtupu..