Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Hivi KWA nn makato ya kibank si rafiki sanaaa,Yani kama wanatuvizia wateja tu tufanye service Kisha ujistukie umelimwa fedha ya maana,KWA nn wasiweke wazi ukifika bank una kuta kila kitu kiko wazi,ama wakutambulishe huduma unayo taka kufanya cost yake ni kiasi kadhaaa.

Mfano NMB,Atm card zao zipo local sana yani ukitumia sana inaanza kusumbua ktk atm,ukiuliza simple wanakujibu ni utunzaji,Ajabu Atm card naweka kwenye wallet KWA bank zote ninazo tumia,ila wao tu ndo haipiti miaka miwili naenda kubadilisha Card,afu makato ya kubadilisha ATM card yapo juu,Baada ya kuomba Atm Kisha uchukulie dirishani ,wanakulima mpaka unakuja juta.
Kubadilisha kadi kama ulifungulia tawi la nje ya mkoa utasikia mhudumu anakwambia tutakata charge tsh 30,000![emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]na vipi kuhusu Standard Chartered?
Wazuri sana kwenye customer care, online banking na security ila makato yao ni hatari tupu. Mimi niko nao kwa sababu ya urahisi wa kutuma na kupokea pesa kutoka au kwenda nje ya nchi pia wana security nzuri kwenye akaunti hivyo si rahisi kuibiwa pesa.
 
Ndugu wasomaji,

Nimeamua sasa kuachana CRDB bank kutokana na makato yasiokuwa na Tija yoyote. Najiuliza, hivi ndio kusema kuweka fedha bank ni utajiti?

Makato yao yanaumiza sana na hayana uhalali wa aina yoyote, haisadi sekta ya bank kukua, mitaji kukua, kukopesha nk.

Nadhani ni wakati wa BoT kuangalia hizi sera za mabank pamoja na huduma zao.

Kwahivyo naona ni bora kutafuta mbadala. Nachoomba ushauri ni bank gani ambayo inatoa online services, mastercard, visa, account activities etc.

Maana kwakweli CRDB wamenishinda. Kupata card, online access ilikuwa ngumu kama kitu gani. Toka Kimei ameondoka naona imekuwa bank ya hovyo sana.
Hii benk ya hovyohovyo Sana,waliniboa hadi hisa nilizokuwa namiliki nikaziuza.
 
Ndugu wasomaji,

Nimeamua sasa kuachana CRDB bank kutokana na makato yasiokuwa na Tija yoyote. Najiuliza, hivi ndio kusema kuweka fedha bank ni utajiti?

Makato yao yanaumiza sana na hayana uhalali wa aina yoyote, haisadi sekta ya bank kukua, mitaji kukua, kukopesha nk.

Nadhani ni wakati wa BoT kuangalia hizi sera za mabank pamoja na huduma zao.

Kwahivyo naona ni bora kutafuta mbadala. Nachoomba ushauri ni bank gani ambayo inatoa online services, mastercard, visa, account activities etc.

Maana kwakweli CRDB wamenishinda. Kupata card, online access ilikuwa ngumu kama kitu gani. Toka Kimei ameondoka naona imekuwa bank ya hovyo sana.
Hizi bank kubwa zina wateja wengi. Kuna wakati naona kama hawajiongezi tena sababu wanajua hatuna options nyingi. Nenda Mwanga Bank...it comes out strong now
 
Hahaa, unakuta mtu akishapata mshara wake akitoa matumizi yake yote balance inabaki 50K, nae anakuambia anasave.
Miaka nenda rudi account haijawai gusa 2M
Account Inashindwa Na Kibubu
 
Equity bank nawakubali kuliko bank zote nchini...naomba tu waongeze matawi na atm ziwe nyingi...wataisoma namba inavoshuka wao watapitisha mishahara lkn hawatakuw na saving ya mtu ..
 
Vipi kuhusu Standard Chartered?
Standard chartered is the best, i do anything as a champ.connected with my tigo pesa and mpesa,i am satisfied for real: Even Absa is the best.chagua brand unayoipenda tu na ujoin,
standard chartered unafungua a feekaunti bure na kadi unaletewa bure na cheque book unapata ukitaka(kwa gharama), Absa kufungua akaunti unaanzia 20000tshs.(kadi unapewa na cheque book applicable kwa gharama) but sometimes cheque book inategemea na aina ya ac.uliochagua mf.personal saving/personal current ac.
Maintanance fees zinarange 5000 hadi 9500 kwa mwezi depends on aina ya ac.uliyofungua. pia unaweza ukaopt. Wazime kabisa online pursase ili hata mtu akiiba kadi yako hawezi kufanya online purchase.pos unaweza fanya kwa sababu inahitaji pin.ni salama.
Equity nao wako vizuri na prepaid card wanazo bila kuwa na akaunti na hawana makato. Except for withdraw
 
Nen
CRDB NI JANGA, kuna tawi pale Arusha linaitwa Usa-River kuna binti yuko kwenye mikopo anaitwa sijui Tarimo D anavyowanyanyasa wateja sijawahi ona. Ukiwa na mkopo wanakuchukulia km jambazi, ni km uliiba. Ikifika tar 22 kila mwezi wanafunga akaunti mpaka tar 27 kila mwezi. Km leo siwezi kuacces A/C yangu mpaka tar 27 kisa nina mkopo pale. Halafu makato hayana fomula, mtu una take home ya sh 1,200,000/ unakatwa mpaka 980,000/ kwa mwezi. Nimejaribu kufuatilia nimeshindwa. Nasuburi muda wao uishe kwa sahv naishi km shetani.
Njoo standard chartered ununuliwe mkopo na ela unapewa uwe malaika. Hadi 150m.
 
Equity iko poa
Nimeshaona matawi yao posta, mwenge, mbagala, temeke, k/koo na maeneo ya pale quality center, na bado gharama za kutoa hela kwa wakala wao bado zipo chini kuliko mitandao ya simu
 
Zinafanana kama vituo vya mafuta, Tanzania hakuna ubunifu hakuna ushindani yaani ukienda Bank moja wakikupa jibu basi wala usihangaike kwenda Bank nyingine ukadhani utapata jibu au huduma tofauti wafanya kazi kwa kukariri tu huduma za wateja ni walewale hawana jipya. mbaya zaidi bank yenye wateja wengi na yenye wateja wachache ni wale wale hakuna ushindani wa ubunifu unategemea mdogo akaja kivingine ile we mkubwa kuvuta watu ila narudi pale pale hawana jipya wala ubunifu.

Wakati mmoja nilidafiri mji mmoja nikafikia Hotel moja nzuri sana tu japo mji ule una Hotel nyingi tu 5 star zinafanana kwa ubora ila hii Hotel kufika pale hujazi chochote unapewa chumba then anakuja yule mtu wa reception na Laptop yake kwa adabu anakuja room anafanya taratibu zote chumbani inakufanya usiwasahu sababu wanakufanya ujisikie Bill gates kumbe huna lolote kubwa huu ni ubunifu kuwa tofauti na wengine.

Ila Tz Bank zote sawa kampuni zote za simu sawa tofauti majina ya ajabu tu ya package zao. Utakuwa Bank inajitangaza sana sasa mteja fika Bank hao customer care utatapika wakati walitakiwa wafanye juhudi wakunase usitoke ili ukienda nje uwatangaze kwa mazuri ndio strategy ya kujitangaza ila ukitoka hapo hata kuangalia nyuma huangalii jioni unawaona kwenye TV Bank bora fika tawi lolote bla bla bla ujinga mtupu..
Ni vile hatuwekezi muda wetu kidogo kufanya research. Tunanunua huduma kwa mkumbo au kusikia.

Standard Chartered, Stanbic, ABSA wapo vizuri sana. Na wapo transparent sana kwenye cost za huduma zao. Huwezi kuta unjustified transactions.

Ila hizi benki zinazopitisha matrilioni ya serikali kaa nazo mbali. Hata ukiondoka wewe hawajawahi kuwaza kama ni wa muhimu kivile.

Nakumbuka wakati natumia fnb, nikideposit mpunga, customer care ananipigia kuniuliza kama nilikutana na changamoto yeyote wakati naweka hela. Nikitaka kudeposit cheque, nawapigia kuwauliza baadhi ya maswali. Ishatokea nilichelewa kidogo bank, nikawapigia wasifunge branch yao ya pale sinza, wakanisubiri. Ila nilichelewa kama 10 mins. Hawa jamaa wapo top kwenye customer care.

Ukitaka ufurahie huduma nzuri, weka pesa kwenye benki ambazo taasisi za kimataifa zinaweka au wahindi wanaweka. Stanchart, Absa, Stanbic, DTB n.k
 
Hata mi kwa sasa Equity ndio nawaelewa!
Uwe unatumia simbanking na atm zingine.

Hao crdb mi sina hamu nao, mwaka huu huu waliwahi kunifanyia mauza uza ambayo sitayasahau, VISA card yangu ilinigomea na ndio acc yangu iliyokuwa na hela na nilikuwa mbalii[emoji852][emoji852] yani ilinibidi nikawatafute hao crdb hadi twitter maana ndio niliona wanarespond haraka, napo wakasema niwatumie email ila mpaka walipokuja kurespond ilichukua muda na haikuishia hapo iliwachukua siku nyingi sana wao kutatua tatizo langu. Kiasi kama nisingekuwa na namna nyingine basi ningeadhirika mchana kweupee,

Toka hapo nikaanza kuithamini acc yangu ya Equity ambayo nilikuwa naidharau mno, kwanza nilikuwa naiwekea tu kama 10,000 kwa mwezi ili tu iwe active, lakini iliniokoa sana
Niliwahama crdb mwaka 2012, card yangu ilimezwa atm ya udsm, nikaenda idai, wakaniambia kwakuwa nilifungua acc mcity, basi nipeleke complaint yangu huko.

Nikafunga acc saa ileile nikasepa.
 
Back
Top Bottom