Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

CRDB siku hizi ni SACCOS, si benki ya kuaminika tena.
Malalamiko ya wengi ni mafoleni yaliyopo, na customer care mufilisi.

Majuzi wameniambia eti nikahakiki particulars zangu.
Nikawuliza nini kimebadilika?
Wakasema we njoo tu!
Nikawaambia siwezi kuja hapo kwa hiari kukaa masaa mawili kusubiri huduma, na nitaifunga hiyo account!
Niliyekuwa naongea naye akashtuka na kusema si hivyo!
Nikafikiri , hawa wanafaya mambo kwa mazoea, wana email yangu na wana simu, kama kuna mabadiliko si watuemie email?

CRDB iliondoka na Kimei!
Hata wakati wa Kimei ilikuwa hovyo tu. Tena ilivyoanza pata tenda za serikali kama nmb ndo ikafia huko.
 
Wanakata mpaka kuangalia salio kwa ATM!! Mi naomba makampuni ya simu yangewakata watu wa benki muda wa maongezi kila wanapotizama salio ili wajue uchungu wake.
Nimeamua sasa kuachana CRDB bank kutokana na makato yasiokuwa na Tija yoyote.
 
Equity bank nawakubali kuliko bank zote nchini...naomba tu waongeze matawi na atm ziwe nyingi...wataisoma namba inavoshuka wao watapitisha mishahara lkn hawatakuw na saving ya mtu ..
Tunaomba . ATM Mbezi mwisho
 
Ndugu wasomaji,

Nimeamua sasa kuachana CRDB bank kutokana na makato yasiokuwa na Tija yoyote. Najiuliza, hivi ndio kusema kuweka fedha bank ni utajiti?

Makato yao yanaumiza sana na hayana uhalali wa aina yoyote, haisadi sekta ya bank kukua, mitaji kukua, kukopesha nk.

Nadhani ni wakati wa BoT kuangalia hizi sera za mabank pamoja na huduma zao.

Kwahivyo naona ni bora kutafuta mbadala. Nachoomba ushauri ni bank gani ambayo inatoa online services, mastercard, visa, account activities etc.

Maana kwakweli CRDB wamenishinda. Kupata card, online access ilikuwa ngumu kama kitu gani. Toka Kimei ameondoka naona imekuwa bank ya hovyo sana.
Mbona mimi sijawah kuomba ku activate kadi zangu za CRDB na mara zote uwa nazitumia kulipia vitu online.
 
Hahaa, unakuta mtu akishapata mshara wake akitoa matumizi yake yote balance inabaki 50K, nae anakuambia anasave.
Miaka nenda rudi account haijawai gusa 2M
Unataka kumaanisha nini mkuu? Wengi mshahara ukitoka akaunti inasafishwa inabaki na negative au frequency za FM radio.
 
Back
Top Bottom