Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Juzi nilitoa kiasi flan salio likabaki vzuri tuu, Jana nmeenda kutoa tena nakuta kiasi Cha elf 20 hakipo, Sasa najiuliza iyo elf 20 imepotelea wap? Ni moja kati ya bank ya ajabu Sana na wanakata pesa bila sababu yoyote nasubiri apa wakanipe maelezo vizuri kabla sijaama iyo bank
Hii Benki imejaa wezi kama mtandao wa Vodacom.
 
Ndugu wasomaji,

Nimeamua sasa kuachana CRDB bank kutokana na makato yasiokuwa na Tija yoyote. Najiuliza, hivi ndio kusema kuweka fedha bank ni utajiti?

Makato yao yanaumiza sana na hayana uhalali wa aina yoyote, haisadi sekta ya bank kukua, mitaji kukua, kukopesha nk.

Nadhani ni wakati wa BoT kuangalia hizi sera za mabank pamoja na huduma zao.

Kwahivyo naona ni bora kutafuta mbadala. Nachoomba ushauri ni bank gani ambayo inatoa online services, mastercard, visa, account activities etc.

Maana kwakweli CRDB wamenishinda. Kupata card, online access ilikuwa ngumu kama kitu gani. Toka Kimei ameondoka naona imekuwa bank ya hovyo sana.
nibora na salama hela zako kubaki nazo nyumbani. tafuta chobingo moja nzuri zitupie huko.Stori za makato utaziskia kwa akina Usokwe na wenzake tu
 
Umezungumzia mambo mawili.
  • Makato
  • Uharaka wa kuhudumiwa /Online Service

Nakushauri fungua account yako na benki ya FNB, kama benki mbadala
  • Account type chagua ile yenye makato fixed kwa mwezi, ni kiasi kidogo, then chochote utakachofanya kwenye account yako hakuna makato.
  • Online Banking wako vizuri, waweza login kwenye account yako kwa simu au PC na kufanya miamala wakati wowote..
Kirefu cha FNB,,?, Je hadi huku nyalikungu wapo?, Maana wamenivutia sana
 
Equaty bank ni nzuri changamoto kwa mikoa mingi Wana tawi moja tuu makao makuu ya mkoa na baadhi ya mikoa hamna kabisa tawi ata mawakala hamna pia Ila Nina account yao na wapo vizuri Sana.
Equity wanasaidia mtu kuwa na nidhamu ya fedha, ATM zao ni za kuhesabu, branch pia, ukienda kwa wakala wengi hawana float.....so ukitaka hela ni lazima uende branch though wanatakiwa waboreshe huduma, waongeze ATM, kuhusu wakala sielewi kwanini wakala wengi wa Equity ukienda wanakwambia hawana float
 
Nmb chachap iko poa sana, haina makato yoyote yaani unaweka bure unatoa bure(ATM) ila tu ni account ya kuweka hela ndogo
 
Vipi kuhusu MKOMBOZI!??

Mimi hawa CRDB nasubiri mkopo uishe tu nitawapotea hawataamini.

CRDB, VODACOM na CCM (ya akina JK, Nape na Makamna) ni WAHUNI na MAJAMBAZI na ADUI wakubwa kwa walalahoi hapa Bongo.
 
Niliwahama crdb mwaka 2012, card yangu ilimezwa atm ya udsm, nikaenda idai, wakaniambia kwakuwa nilifungua acc mcity, basi nipeleke complaint yangu huko.

Nikafunga acc saa ileile nikasepa.
Wapuuzi sana, huduma mbovu kabisa
 
Back
Top Bottom