Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

njoo nmb kidogo wana nafuu naweza kutoa mfno 500k nkakatwa mpka buku 2 tu kwenye ATM

kingine nachopendea ni ukiwa na app yao kucheki balance ni bure bas nikiwa na vijisent vyangu kila nikitoa hela lazma nihakiki mzigo wangu to be honest kwa hilo naenjoi nao
 
Naona tumezoea kukatwa sasa. Yaani mtu kukata pesa yako uliyompa afanyie biashara tunaona kitu cha kawaida! Yeye ndiye anayetakiwa akupe faida. Kutoa pesa ni huduma ya kawaida ambayo inatakiwa iwe bure.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mpaka sasa options za banks nimeona hizi ndo zimekua suggested mara nyingi..


1. Equity (Ki ukweli hawa niko nao miaka sasa wako vizuri makato kidogo hata customer care yao online wanajibu haraka sana, japokua mapungufu wanayo ya kutokua na matawi mengi..)

2. FNB

3. ABSA

4. Standard Chartered Bank

5. Exim

6. NMB Chap chap account ( Hii kwa wenzangu na mimi wa pesa za madafu inatufaa haina makato makubwa pia haina fee charges za mwezi, inafaa kwa kuweka pesa ndogo)

Ni hivyo tu kwa ku summarize..
 
Nmb ni wale wale tu hawana tofauti kubwa na CRDB . Hapa nimeshawishika kweli kujiunga na Equity Bank
 
Kwahiyo kumbe nikicheki salio kwa Sim banking app ya CRDB huwa ninakatwa bila kujua??
 
KCB ndio naoan Bank inayo fanya vizuri sn katika kila nyanja sema mahati mbaya ni kutoka KENYA tu lkn ndio Bank Bora kwa sasa.

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app

Hata Equity ni ya Wakenya. Banks za wakenya kwa sasa zinafanya vizuri sana Hapa Tanzania. Wamejua udhaifu wa hizi banks zetu wameufanyia kazi fasta. Wabongo itabidi wajifunze kwa wenye hizo Bank.
 
Hata Equity ni ya Wakenya. Banks za wakenya kwa sasa zinafanya vizuri sana Hapa Tanzania. Wamejua udhaifu wa hizi banks zetu wameufanyia kazi fasta. Wabongo itabidi wajifunze kwa wenye hizo Bank.
Shida ya hizo banks hazijasambaa vizuri, na watu wengi wanaangalia urahisi wa ku-withdrawal pesa kupitia ATMs. Mambo ya kwenda kupanga foleni ili kutoa pesa yanahitaji commitment.
 
Nilihamaga crdb toka kipind niko chuo miaka ya mwshon kisa vimakato tena makubwa ambayo hujui kwann wamekata mzee inauma hela unayoitegemea ya mawazo unakuta wamefyeka kama slesha kwenye nyasi[emoji23][emoji23][emoji1787]
 
CRDB wenyewe ni majambazi, alafu tena wameajiri vibaka na majambazi wenzao. Mnapeleka pesa kwa vibaka na majambazi, mnategemea nini?
 
Nenda TPB,ABSA, EQUITY hawakajawahi Niangusha wako vizuri mnooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Benki ya Posta ni bora kwako!
 
Au nenda benki yoyote ya Kiislam, maana nasikia wao masuala ya riba ni haramu kwao!
 
Kadi yangu ya CRDB ilipotea, eti kupata nyingine sh 23800 niliwahama siku hiyo hiyo
CRDB hawako open kwenye gharama za huduma zao.
Sasa kuhusu hela zako banki ulifanyaje, au kulikuwa na salio lile la kinda mfuko la elfu tisa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…