Kuna mchizi wangu job! Alitia mimba dem wa kichaga mwaka jana, lkn alikua ashaona hawawezi kukaa pamoja kwa sababu demu mzito sana kwenye mipango ya maisha. Yaani ni yule dem akija getto hawezi kugusa chombo aoshe au apike, yy akija anataka waagize chips kuku wacheki movie, na kumpa mtonyo wa kusuka, dem alikua kamaliza chuo mwaka huo huo. Maza ake alivyogundua dem anamimba, na aliyempa mimba ana ka kazi ka maana, akaanza kumsumbua mchizi aende kujitambulisha. Akapiga chenga sana hadi akaenda. Kufika wakapanga na mahari kabisa mil 2.
Dogo alipojifungua tarehe za mahari zikawa zishafika, jamaa akawa anatia kalenda, ooh hali mbaya, nivumilieni bado najipanga, hahaha: ilifikia hatua maza ake na dem kamtia dem kwenye gari kampigia simu jamaa kumtaarifu mkeo na mwanao Wanakuja huko mlee pamoja kama ni kujipanga mtajipanga mkiwa wote. Mkitaka kuleta mahari ni nyie.
Ko kiufupi hii mambo ya kujipanga inategemea na mtazamo wa wazazi wa dem. Vinginevyo mzigo utakomaaa nao hadi uchoke.