Ninahisi nina kichaa, tafadhali nisaidieni, msinikejeli wala kunisema...

Ninahisi nina kichaa, tafadhali nisaidieni, msinikejeli wala kunisema...

Umejifungia miaka mitano unakula nini?
 
Kichaa hawezi kujitambua yeye ni kichaa Mkuu.

Watu wengi wapo Kama wewe, hiyo ni moja ya athari za utandawazi na kukua Kwa Miji.

Zingatia, upweke Unaua, tafuta mke kisha OA upate challenge za kikubwa ili walau uwe mtu mzima mwenye majukumu
Kwa huo ukichaa huyo mke atapata shida sana, aende tu clinic za phycology awaelezee hata kama ni mbali lipa gharama za nauli na hotel nenda utapata huduma nzuri sana na matibabu ni siku moja tu unapewa dawa unakwenda kutumia alafu unapangiwa tarehe za kuwa unahudhulia clinic mpaka unapona hilo tatizo.
 
kwa hizi dalili wewe sio kichaa,ila una tabia ambazo unatakiwa kuzibadili.INAWEZEKANA.
IMG_20220610_190828.jpg
 
Kumbika kasema akikumbwa na changamoto anakua na hasira sana.

Akioa huyu ni rahisi kuua au kujeruhi akipata mashaka juu ya mkewe hata kidogo tu.
Ni kweli kabisa, asioe kabla ya tiba, tuna mtu wa hivyo katika famiia alioa kabla ya tiba ikawa shida wanawake wakawa wanakimbia ila baada ya tiba amepona ila dalili hatarishi zikimutokea anawasaliana na daktari wake pia watu wa hivyo wanapata ugonjwa wa presha mambo yao yasipokwenda wanavyotaka hivyo clinic ya magonjwa ya akili ni muhimu kwao.
 
Pole sana ndugu yangu......na hongera kwa kutambua tatizo lako na kutafta suluhu.....nakushauri nenda hospitali upate msaada wa wataalamu wa afya....jitahidi pia utafute msaada kwa viongozi wa kidini upate dua na maombi utakaa sawa

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kumbika kasema akikumbwa na changamoto anakua na hasira sana.

Akioa huyu ni rahisi kuua au kujeruhi akipata mashaka juu ya mkewe hata kidogo tu.

Watu wapweke ndio tabia zao hizo 😀😀
Hasira za kipuuzi wanakuwaga nazo.

Hata mume au mke aliyeolewa lakini mwenza wake Hana time Naye baadaye hujihisi upweke na matokeo yake huwa na kisirani, Gubu na hasira za kijinga.

Hili lipo zaidi Kwa wanawake walioolewa alafu wakawa hawapewi attention na waume zao hujihisi upweke na kujikuta na mahasira ya kijinga
 
Mpaka unadhani una kichaa basi ujue hauna kichaa.

Huwezi kuwa kichaa alafu ukajijua kuwa una kichaa.

Anyway, usiogope, kila mtu ni kichaa ila kichaa kinatofautiana.

Iwapo kila mmoja wetu kwa nyakati tofauti amewahi kufunga mlango akalala, ila baadaye akahisi hajafunga, na kuamka tena kukagua na kukutwa umegingwa, basi hii ni dalili ya ukichaa

Basi mim kichaa aisee
Naendaga kukagua mlango hata mara tatu kama nimefunga
 
Habar wana jamii, kwanza nianze kwa kusema mm ni mtu mwenye hasira sana, ninasumbuliwa na depression napenda kujiisolate na kukaa mwenyewe, tangu nimalize chuo sikutafuta kazi nimejifungia ndani huu mwaka wa tano, sikuwa naelewa tatizo langu nini Ila nimejua mwaka Jana kuwa shida ni mental health

Tangu nikiwa mdogo sikuwa na ushirikiano na wenzangu na haswa pale nilipokuwa nikikutana na changamoto ninapata hasira mbaya sana.

Sijawahi kumwambia mtu coz sina mtu wa karibu wa kumweleza na mm ni msiri sana which I think inatokana na kuwa na ukichaa pia, je kuna dawa yoyote inayoweza nisaidia sehemu nilipo hamna mental hospital.
Tafuta demu tu ndio dawa yako
 
Unapata tabu bure,

Hatuwezi wote kufanana......... hata hivyo.

Kujielewa na kubalansi uhalisia tu ndio muhimu. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa jinsi mbalimbali ili tutumikiane na tukamilishane.
 
Dah pole Sana mkuu, kweli una tatizo. Miaka 5 upo ndani bila kuchakarika???. Halafu mtoto wa kiume. Embu tafuta marafiki kwanza uchangamane nao...
 
Jamaa ni kichaa kwa kujiongezea,yani kasoma chuo kapaform fresh halafu aende kujifungia ndani

Angekuwa usukumani tayari angekuwa keshaitiwa masungusungu kwa kuhisiwa mwibhi
Kwan usukuman ukijifungia ndan wanakuitia mwizi?
 
Back
Top Bottom