CHADEMA wameshikilia hoja yao ya kufanya maandamano kesho. Serikali pia imeshikilia msimamo wake pia kuwa kesho hakuna maandamano. Serikali ina hoja ya kwa kutokea uvunjifu wa amani na CHADEMA pia wana hoja ya kutaka vijana wao waliotekwa waachiliwe huru au warudishwe wakiwa wamekufa. Mfano kama CHADEMA wakishikilia msimamo wao kesho kunaweza kutokea maafa makubwa ambayo haijawahi kutokea kwa sababu hawawezi kushindana na serikali na lawama zote zitaelekezwa kwa Serikali hasa kwa Mhe. Rais. Rai yangu kwa Serikali hasa kwa Mhe. Rais wakae meza moja na CHADEMA ili muafaka upatikane ili kuwe na win win situation vinginevyo yatakayo tokea kesho itakuwa nimaafa makubwa.