Ninajua kila mtu anajua kinachoendelea kule Los Angeles ila sijui ni wangapi wanajua chanzo cha ule moto unaouangamiza mji wa uzuri wa Dunia

Nyumba nyingi za huko L.A zimejengwa kwa mbao, ni rahisi kuungua.
Hasara ni kubwa kwenye mali na sio uhai wa watu, mpaka jana walio lipotiwa kufa ni 24 tu!
Wamekufa wachache kwa taarifa ya serikali.. Sitaki kuhoji ukweli wake... Kwa wengi wasioijua marekani wana viwango vya juu sana vya usalama kwenye kila kitu
 
Nimekwambia binadamu tunazaliwa.

Binadamu hatujaumbwa.

Unataka nikuthibitishie mola hayupo wakati wewe unayedai yupo huna uthibitisho.

Kuzaliwa ni tokeo la mwisho kabisa, mbona unajitoa ufahamu ?

Angalia asili ya mwanadamu nini ? Ni muunganiko wa mbegu za kike na kiumu, hapo ndio uumbaji unapoanza.

Naam, lazima uthibitishe juu ya kutokuwepo kwa Mola, sababu wewe una dai hilo. Shida yenu huwa mnaona ya kuwa jukumu la kuthibitisha ni la yule anae sadiki na sio nyie mnao kanusha. Hii akili ya uoga na uchachefu wa maarifa.

Usikimbie hoja.
 
Wewe unakipi unachojua?

Unakipi ulichofanya kuleta maendeleo kwenye hii dunia?

Serikali yako tu, inategemea mikopo na misaada ya hao wazungu.

Halafu wewe unakuja hapa kusema wazungu ni wajinga.

You need mental rehabilitation therapy.

Vichache ninavyo jua kuliko vingi nisivyo vijua, Moja wapi ya vichache Nina vyojua ni la uwepo wa Mungu.

Nina vingi sana nimefanya katika hii Dunia.

Hizi nukta za tatu za mwisho zinaonyesha mada imekushinda na Mimi sishughuliki nazo.
 
Umegundua nini katika hii dunia hadi useme wazungu ni wajinga? wakati kila kitu unachotumia wamekigundua wao?

Hujui ulimwengu wa kielimu, soma gunduzi nyingi ambazo zimebadili hii Dunia hawajafanya wazungu.

Wazungu WAJINGA kwenye vingi bali ni waongo sana, isipokuwa wale ambao Allah amewarehemu, hata hiyo Sayansi unayo Iona wewe ina makosa mengi.

Kutogundua jambo haimaanishi walio gundua mambo wanaakili sana. Mfano mwepesi hivi unaelewa nini ukiambiwa Kuna mzungu aligundua Mlima Kilimanjaro au Ziwa Victoria ? Je ni kweli aligundua au aliliona kisha akatoa jina ? Je hapo kabla hawakuwepo watu wakiishi eneo hilo ? Wenyeji waliitaje eneo hilo ? Sasa tofautisha kati ya kugundua na kutoa majina.

Kingine, sio kila kitu nachotumia Mimi wamekigundua, kingine nakupa kazi nenda kadurusu upya tamko "Kugundua".
 
Kwa Imani yako ni yeye ndio aliwatengeneza na kuwaleta kwahio alitegeneza wajinga na wazembe ili aje awalipue ili iweje ?

Allah ameumba hajatengeneza, jifunzeni maana za maneno na mjue mipaka yake, ili msikosee katika kujenga hoja.

Allah aliumba ujinga na weerevu, ndio maana ukiamua kuwa msomi unakuwa na ukiamua kuwa mjinga unakuwa mjinga vile vile.

Kwahiyo Allah hajaumba mtu awe mjinga au awe mwerevu, bali ameumbwa ujinga na werevu kisha ukapewa uwezo wa kuvidiriki viwili hivyo au kutovidiriki.

Kwahiyo chaguo ni lako.
 
Basi, Allah ni dhaifu sana

Huo ndio ukamilifu Sasa, sababu anawaweka wote na mwisho wa siku anawachambua na kuwapa stahiki zao.

Lakini hilo kwake ni dogo anaweza akamtoa mtu katika janga lililo wakumba wengi na wengi wakashangaa imekuwaje huyu kapona. Huu ni utaratibu wake.

Shida yenu mnajadili msiwe mjua, na hapa mtaendelea kukosea mpaka mnakufa.

Kingine, Allah Kuna mambo amejiharamishia na amejiwekea taratibu zake ambazo hazibadiliki.

Lakini, Kuna maombi pia nitumie wake walimuombea juu ya nyumati zake.
 
Calfonia nzma wapiga kura walikuwa 15 tu? Sasa hap wapiga kura wamekufa?
 
Game plan tu hizo, watu wa kanisa wanatumia kama opportunities kuendelea kuwapiga wajinga kwa issue ambazo zimepangwa na wa U.S kwa manufaa ya U.S
 
Mungu zero (0) kaamua muachia mungu wa dunia hii awafundishe kwamba mie huwa natamba huku Baba akiwa pembeni sasa mmemfukuza sasa maji mtaita mma
 
Ni kweli;
MUNGU HADHIHAKIWI.
 
When rational fails we turn to spirituality...

By the way kama huyo Mungu waliyempa Sifuri anaghadhabu na visasi kiasi hiki nadhani walikosea wangempa kabisa Negative.., na wako sawa kutaka kukaa nae mbali kabisa.
Nenda kawaambie; kama hawajakutoa nduki.
 
Ukistaajabu ya LA, usishangae yatakayozikumba big cities za EA.

Muda umefika wa kumkubali Mungu au kumkataa ufe Kwa majanga.

Unabii wa Mathayo 24 unaendelea kutimia kuhusiana na miaka 7 ya kufa na kupona. Katika kipindi hiki, yatatokea mambo ambayo hayatakuwa ya kawaida, Nia ni kuwakumbusha watu wamrudie Mungu na kujiandaa Kwa UNYAKUO wa Kanisa.

Ni 2023-2030.
 
Kwa upande mwengine huo moto ni mipango yao binafsi ili waubadilishe huo mji wa LA kuwa smart city 2030,pia housing insurance wali cancel ili wasipate hasara pindi tu janga la moto litakapo anza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…