Ninakemea uongo, uzushi na fitna kwa Rais Samia. Wote mnaokosoa hamtafanikiwa

Ninakemea uongo, uzushi na fitna kwa Rais Samia. Wote mnaokosoa hamtafanikiwa

Hawa ni wapuuzi wa kupuuzwa, Bora mama Sasa aminye tu uhuru wa habari, maana hawa kenge hawana shukrani
Kwa nini asianze kukiminya hicho kichwa chako kwanza ili kiwe na akili sawa na sisi binadamu wenzako? Maana kwa sasa akili zako hazina kabisa tofauti na zile za kuku 🐔 eti!!
 
Mama Samia anapaswa kutiwa moyo na kumuombea kwa Mungu amuongoze vema. Watu watake ama wasitake, mama Samia ni Rais na katiba inamtambua hivyo.
 
Mosi Hebu tupe majina ya wanaolipwa kuikosoa serikali..

Pili tupe ushahidi wa kimaandishi kuonesha hayo malipo ya kuikosoa serikali yanatokea kwa nani kwenda kwa nani na kwa njia ipi ya malipo...

Tatu tupe mkataba unaoonesha namna wakosoaji wamepewa namna ya kukosoa na unadumu kwa muda upi maana ukosoaji uko duniani kote na hakuna asiyekosolewa..
Hii nchi imejaa wapumbafu sn, ukitoa ushauri au kukosoa unakuwa unalipwa
 
Dawa ni hawa Maraisi wawe wanaiba ili wasije kunyanyasika huko mbeleni watu wanakomaa na Sedan la kuendea Mkuranga.
 
Maswali ya kipuuzi kabisa haya
Kama hawalipwi ni nini kinawawasha kukosoa hata ambavyo havikosoleki?
images (47).jpeg
unaweza ukadhani ni nchi tofauti kumbe nchi ambayo Ni masikini wagonjwa wanalala chini bado inampa mzee wa miaka 96 zawadi ya gari la bei ya kutupwa.....

Nchi ambayo viongozi wake wanatembelea gari ya millioni 400 huku wajawazito wakilala chini na bado wakiambiwa zaeni tu

images (44).jpeg


images (45).jpeg


images (48).jpeg


images (49).jpeg
 
Ngoja tuulize ma auditor ni pesa kiasi gani ya umma inayotakiwa kutumiwa kinyume na utaratibu unaofaa....nasikia kipindi fulani pesa ya umma hata iwe ni jero maelezo yake yakikosekana hata kama unao uwezo wa kuirudisha papo kwa hapo ilikuwa ni mshike mshike kwenda kunyea debe...
 
Unasema Na kuutetea, kwa namna moja upo sahihi na kwa upande mwingine huenda ukawa haupo sahihi, sambamba na hao wazungumzaji juu ya hayo unayoyasema huenda wakawa sahihi au wasiwe sahihi.

jambo la kujiuliza ni, je kulikuwa na ulazima wa zawadi hiyo iliyotolewa kwa gharama ya namna ile? Kama jibu ni ndiyo basi mama na apongezwe.

Serikali imewezaje kutatua kero za wastaafu walioitumikia nchi kwa miaka mingi japo wa 4 tu ambao hawajalipwa fedha zao na madai yao hayafikii thamani ya zawadi? Kama jibu ni serikali imetekeleza basi mama na apongezwe.

Mwisho si kila aikosoae serikali ana chuki nayo, kuna msemo unasema mwenye macho haambiwi tazama.
 
Leo imenibidi niliongee hili ili niae huru kwa maana moyo unauma kuona uongo uzushi chuki na fitna kwa Mama Samia.
Ninaona ni Kama watu wamejipa ajira ya kudumu ya kukosoa maraisi. Kukosoa sio dhambi Ila inategemea na unachokosoa.
Hadi Sasa sijaona Kama Kuna jambo la kumkosoa Mama Samia, nasema SIJAONA KABISA.
Kuna watu pengine wanalipwa kwa kuikosoa serikali, hivyo serikali ifanye vizuri au vibaya wao wanakosoa tu.
Sasa jiulize unamkosoa mama Samia kwenye lipi? Ni kipi kakosea hadi Sasa hadi muanze midomomidomo?
Mara sijui kwa nini avunje vibanda, Sasa Kama kaona hawafati Sheria kwa nini asivunje?
Mtu anakurupuka anasema ooh kwa nini sijui kampa mwinyi gari, gari kweli? Tena kwa raisi mstaafu ni issue?
Wengine ooh sijui kasababisha mechi isichezwe? Akili za namna gani hizi? Ikatokea ukakutana na kibaka huko mtaani akakukaba utasema pia mama Samia ndio kamtuma?
Hakuna mwenye hoja kabisa ya kukosoa zaidi ya ushabiki tu. Tuache ushabiki tuchape kazi
Wanaojiita wanaharakati na yule jamaa yenu mliekuwa mnamuabudu kule twitter nao kila siku wanatafuta kwa nguvu la kuzusha ili tu Mama Samia aonekane hafai, sijui wenzetu walisaini mikataba ya kukosoa serikali?
Unamkosoa Mama Samia kwa lipi baya? ACHENI hizo, Ila tutaenda sawa maana kukosoa mnasema ni Uhuru wenu Ila hata sisi kuwakemea nyie ni Uhuru wetu
Mama Samia kanyaga twende...............!!
#kazi iendelee#
Kuwa mwanaharakati sio basi kila jambo wewe kupinga tu wakati mwingine penye mazuri unasema ukishakuwa wewe basi kukosoa tu hata zuri unakosoa eti mwanaharakati. Wakati wa JPM wote hawa walikuwa wameufyata sasa naanza kuelewa kumbe JPM aliwajuwa hawa bila fimbo hawaendi. japo sijawahi kuwa fan wa JPM lakini nilikuwa namkosoa nayoona mabaya lakini penye mazuri nilimpa sifa zake. Mama Samia pia yako atawakwaza watu na yako atafanya mema. Mama fanya kazi kwa nia njema mengine ya huku waache kikubwa imani yako na nia yako kufanya mazuri.
 
Hii nchi imejaa wapumbafu sn, ukitoa ushauri au kukosoa unakuwa unalipwa
Ndio mnaliowa, Sasa Kama hamlipwi mnawashwa na nini? Ndio kwanza mwezi mmoja tu Ila ujuai mwingiii
 
Kasema waziri walifanya vibaya wabunge wawakosoe vikali.
Sijui kusoma Hamjui?au wewe ni mbunge?
Sasa ni rasmi wewe ni Zuzu tu kama mazuzu wakubwa wa Lumumba kina Jingalao na Elitwege. Kwa hiyo katiba inataka Rais akosolewe na Wabunge pekee? Weka Ibara hapa tuisome.
 
Kuwa mwanaharakati sio basi kila jambo wewe kupinga tu wakati mwingine penye mazuri unasema ukishakuwa wewe basi kukosoa tu hata zuri unakosoa eti mwanaharakati. Wakati wa JPM wote hawa walikuwa wameufyata sasa naanza kuelewa kumbe JPM aliwajuwa hawa bila fimbo hawaendi. japo sijawahi kuwa fan wa JPM lakini nilikuwa namkosoa nayoona mabaya lakini penye mazuri nilimpa sifa zake. Mama Samia pia yako atawakwaza watu na yako atafanya mema. Mama fanya kazi kwa nia njema mengine ya huku waache kikubwa imani yako na nia yako kufanya mazuri.
Bila fimbo hawaendi Hawa. Mama Samia chapa fimbo hawa
 
Back
Top Bottom