Ninakubaliana na Rais hakuna vita ngumu kama ya uchumi, tushikamane

Maisha ni uchumi na uhuru wa kweli ni uchumi. Wale waliosomea siasa Uchumi yaani political Economy wanajua uhusiano wa siasa na uchumi. Pia wanafahamu uhusiano wa binadamu juu ya uzalishaji.

Kimsingi mapambano yoyote ya kisiasa msingi wake ni uchumi ni nani apate nini na kwa wakati gani. Taifa letu linapita kwenye kipindi kigumu kutokana na jitihada za Rais wetu kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kulifanya taifa kujitegemea na kwa kulinda raslimali zake.

Hivyo vita vya ndani na nje ya nchi kama taifa na Rais wetu ni matokeo ya jitihada hizo na matamanio ya kundi la ndani ya nchi kushirikiana na mataifa nyonyaji nje.

Kihistoria kuanzia wakati wa biashara ya utumwa, ukoloni na sasa ukoloni mambo leo Afrika imekuwa mhanga wa ukandamizwaji na mataifa makubwa kunufaika na raslimali ipatikanayo Afrika.

Fika ulaya ujionee ilivyojengwa kwa raslimali zetu na biashara ya utumwa enzi hizo.Mataifa haya hayataacha kupigania kututawala kiuchumi yakijua raslimali iliyopo ni muhimu kwa mustakabali wa mataifa hayo.

Kelele tunazosikia kwenye siasa ndani na nje ya nchi ni vita ya kiuchumi. Hivyo watanzania tushikamane na Rais wetu dhidi ya unyonyaji huu.

Aidha vyombo vya dola, serikali na mifumo yote haina budi kujengwa upya kwa mwelekeo wa falsafa ya kizalendo na kujitegemea ili kukabiliana na vita hii ambayo hujitokeza katika sura na mbinu mbalimbali zisizo na kikomo.
Yaani vita ya kiuchumi ndio inawaelekeza muuwe watu na kuiba kura kwenye uchaguzi??
Na bado mtapata mbinyo mpaka mkojoe dagaa
 
Ulaya imejengwa na wenyewe acheni kujidanganya kuwa kila kitu kipo Tz kuanzia madini sijui na ujinga gani? Vita ya uchumi kwa hapa nchini inaletwa na CCM na viongozi wake kuibia wananchi

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Tuko kwenye vita ya kiuchumi na nani? Hiyo vita imeanza lini? Kwanini?

Sio kila mnaloambiwa mnameza hivyo hivyo, Tz inaingiaje kwenye vita ya kiuchumi na nchi kama USA? Ukiona yanayoendelea kati ya China na US ndio unaweza kupata uhalisia wa nini maaana ya vita ya kiuchumi!

Sisi hapa sanasana tunasmweza kuingia kwenye vita ya kiuchumi na laabda Kenya, tuseme kwa kugombania wateja wa bandari!
Vita ya kiuchumi ni suala la kihistoria kwa nchi za magharibi kunufaika na raslimali zetu kwa bei nafuu, kuhamisha madini, biashara isiyo sawia na kwa mwendelezo wa kuifanya Afrika soko lao na sehemu ya kuchuma au kodi za tax holidays etc. Hivyo ukiweka mifumo ya kuwadhibiti au kujiimarisha mwenyewe mapema ki nchi lazima makampuni yao yapige kelele na hiyo ndiyo vita yenyewe inaanzia hapo. Huo ndio ukweli upende au usipende.
 
Maisha ni uchumi na uhuru wa kweli ni uchumi. Wale waliosomea siasa Uchumi yaani political Economy wanajua uhusiano wa siasa na uchumi. Pia wanafahamu uhusiano wa binadamu juu ya uzalishaji.

Kimsingi mapambano yoyote ya kisiasa msingi wake ni uchumi ni nani apate nini na kwa wakati gani. Taifa letu linapita kwenye kipindi kigumu kutokana na jitihada za Rais wetu kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kulifanya taifa kujitegemea na kwa kulinda raslimali zake.

Hivyo vita vya ndani na nje ya nchi kama taifa na Rais wetu ni matokeo ya jitihada hizo na matamanio ya kundi la ndani ya nchi kushirikiana na mataifa nyonyaji nje.

Kihistoria kuanzia wakati wa biashara ya utumwa, ukoloni na sasa ukoloni mambo leo Afrika imekuwa mhanga wa ukandamizwaji na mataifa makubwa kunufaika na raslimali ipatikanayo Afrika.

Fika Ulaya ujionee ilivyojengwa kwa raslimali zetu na biashara ya utumwa enzi hizo. Mataifa haya hayataacha kupigania kututawala kiuchumi yakijua raslimali iliyopo ni muhimu kwa mustakabali wa mataifa hayo.

Kelele tunazosikia kwenye siasa ndani na nje ya nchi ni vita ya kiuchumi. Hivyo watanzania tushikamane na Rais wetu dhidi ya unyonyaji huu.

Aidha vyombo vya dola, serikali na mifumo yote haina budi kujengwa upya kwa mwelekeo wa falsafa ya kizalendo na kujitegemea ili kukabiliana na vita hii ambayo hujitokeza katika sura na mbinu mbalimbali zisizo na kikomo.
Ujinga wako mkubwa.
 
Happy
Kwa hiyo vita ya kiuchumi ndio inawaelekeza muue watu, mteke, muwabambikie makesi, mpole uchaguzi, muengue wagombea wa upinzani na mpitishe wa kwenu bila kupingwa?

Kwa akili hizi Bora wazungu wawanyooshe kweli ili mjifunze kueshimu utu na ubinadamu wa w

Happy wazungu unaowashabikia watatunyoosha sisi akina Nani. Na watatunyoosha kivipi...na wewe ni Mkenya kwani haliwezekani uwe mtanzania kwa kufurahia baadhi kunyooshwa
 
Mie ni mtanzania na ndo mana siwezi kufurahia watanzania wenzangu kuuwawa, kutekwa, kubambikiwa kesi na haki zao kupitia sanduku la kura kunyang’anywa
 
Ni Nani waliouawa, kutekwa na kubambikiwa kesi...wauaji ni Nani...na watekaji ni akina Nani...Sasa hao wazungu unataka wawanyooshe akina Nani? Na wakinyooshwa hao wewe utanufaika vipi?
 
Ben Saanane, Azory Gwandwa, Rwabaje, watu wa mkuranga 400. Kaka wa wenje, wanachadema singida na wafuasi wa ACT Zanzibar. Wauaji na watejaki ni vyombo vya ulinzi na usalama vya Jiwe wakuu wa izo taasisi na boss wao ambae ndo unaemtetea humu ndo watanyoshwa na wazungu
 
Ok ok Hilo la sijui Ben Saanane, Gwandu huwezi kutupa lawama kwa vyombo vya dola kwani hakuna ushahidi...Hilo la watu 400 wa kibiti inaelekea unazo taarifa nyeti peleka polisi...ila huko Kibiti usisahau mauaji ya watu wa serikali na CCM na pia polisi ..je unayo majina ya watu hao 400 unaodai waliuawa? Wanachadema huko Singida na wafuasi wa A CT wazalendo je walikuwa wanafanya Nini mpaka yawakute yaliyowakuta...usisahau pia mauaji ya makada wa CCM kule Njombe na Tunduma nalia kuchomewa nyumba Kibaha na kwingineko...wakati tunaomboleza vifo vya wote ni vizuri uelewe ndani ya Chadema na pia ACT Wazalendo Kuna magaidi...Askari polisi amechinjwa huko Pemba na makada wa CCM wanauliwa na wauaji ni wafuasi wa Chadema na Sasa ACT Wazalendo...
 
Ili kushinda vita ya kiuchumi lazima ujenge jeshi lako, ambalo ni wafanya biashara, na ndio sababu viongozi wakuu wanapoenda kwenye nchi zingine wanakwenda na wafanya biashara, sasa sijui kama hilo lipo, kwani biashara zinafungwa, kesi za uhujumu, serikali ikishajenga hofu kwa wafanyabisha hakuna uchumi, kwani makosa yapo sana kwenye biashara, ni kama mwanajeshi aliyeko vitani kuna makosa mengi yanafanyika kotokana na mazingira. hivyo serikali inatakiwa kujadiliana na kumaliza makosa hayo mezani, ni kama Trafic case, kama zingeshughulikiwa kama mada kesi nazani hakuna mtu angetaka kuendesha gari. Ili tuendelee Kiuchumia ni lazima tuwe na viongozi amabao wanaipenda nchi yao na wanaona aibu kuongoza watu masikini.

Ukichagua kiongozi aliyeathirika na umasikini ni ngumu Sana kusonga
 
  • Thanks
Reactions: Lob
Maisha ni uchumi na uhuru wa kweli ni uchumi. Wale waliosomea siasa Uchumi yaani political Economy wanajua uhusiano wa siasa na uchumi. Pia wanafahamu uhusiano wa binadamu juu ya uzalishaji.

Kimsingi mapambano yoyote ya kisiasa msingi wake ni uchumi ni nani apate nini na kwa wakati gani. Taifa letu linapita kwenye kipindi kigumu kutokana na jitihada za Rais wetu kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kulifanya taifa kujitegemea na kwa kulinda raslimali zake.

Hivyo vita vya ndani na nje ya nchi kama taifa na Rais wetu ni matokeo ya jitihada hizo na matamanio ya kundi la ndani ya nchi kushirikiana na mataifa nyonyaji nje.

Kihistoria kuanzia wakati wa biashara ya utumwa, ukoloni na sasa ukoloni mambo leo Afrika imekuwa mhanga wa ukandamizwaji na mataifa makubwa kunufaika na raslimali ipatikanayo Afrika.

Fika Ulaya ujionee ilivyojengwa kwa raslimali zetu na biashara ya utumwa enzi hizo. Mataifa haya hayataacha kupigania kututawala kiuchumi yakijua raslimali iliyopo ni muhimu kwa mustakabali wa mataifa hayo.

Kelele tunazosikia kwenye siasa ndani na nje ya nchi ni vita ya kiuchumi. Hivyo watanzania tushikamane na Rais wetu dhidi ya unyonyaji huu.

Aidha vyombo vya dola, serikali na mifumo yote haina budi kujengwa upya kwa mwelekeo wa falsafa ya kizalendo na kujitegemea ili kukabiliana na vita hii ambayo hujitokeza katika sura na mbinu mbalimbali zisizo na kikomo.
Vita ya uchumi,sio kuiba mali ya umma,mnajenga shule za kata,mnasema Elimu ipo vzr,lakini hakuna mtoto wa waziri anayesoma shule za kata.
 
Back
Top Bottom