Administer
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 2,639
- 2,384
NDUGU YANGU NI KAWAIDA WACHAMUNGU NA WASIOWACHAMUNGU HULITEJA JINA LA MUNGU,WAOVU NA WEMA WANALITAJA JINA LA MUNGUKwa lipi hadi utaje taje Jina la Mungu?
1. Kagera walipopatwa na tetemeko uliwaambia kuwa CCM wala Serikali hawajaleta tetemeko. Hiyo siyo kauli ya mtu anayemcha Mungu.
2. Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi wewe kama kiongozi wa kitaifa hujawahi kuja na hatua yoyote dhidi ya tukio hilo. Huo siyo mwenendo wa mcha Mungu.
3. Walipotaka kukusanyika ili wamuombee Tundu Lissu uponyaji wa haraka ukawazuia. Huo siyo moyo wa mcha Mungu.
4. MO Dewji alitekwa akarudishwa akiwa amedhalilishwa. Wewe kama kiongozi wa kitaifa hukumuwajibisha yeyote kutokana na tukio lile. Huo siyo mwenendo wa mcha Mungu.
5. Ben Saanane na Azory Gwanda wenye familia zinazowategemea wamepotea na kupotea. Wakati familia zao zikilia hakuna chochote kinachoendelea. Kiongozi mcha Mungu kweli angeonekana hata kwa haya yaliyotokea.
6. Chini ya utawala wako watu wamepelekwa mahabusu kwa upelelezi usioisha, wamepewa kesi zisizo na dhamana wamo pia vijana wadogo, viongozi, wanasiasa. Kisha kwa mapenzi yako ukawaachia huru wafungwa wa ulawiti na ubakaji. Huo siyo mwenendo wa mcha Mungu. Mcha Mungu anatenda haki kila sehemu, habagui kwenye kutenda haki.
7. Unaruhusu anasa wakati wa janga la Corona, watu watanzania wanapimwa huko mipakani na kurudishwa nchini, wapo wanaokufa mpaka leo. Ukiacha anasa zikaendelea wakati wa janga kisha unarudi na kusema kuwa Mungu katuondolea janga mbaya zaidi ukiwa na lengo la kuuficha ukweli fulani kwa hakika Mungu huyo anaweza kukupa pigo la aina yake.
Mwisho niseme tu kuwa kiongozi mcha Mungu hafichi fichi mambo kwa manufaa yake kisiasa. Ni mkweli kila upande. Hachagui upande wa kuongea ukweli wala wa kuficha ukweli. Ukimuangalia leo yake ni sawa na jana yake na vile vile ni sawa na kesho yake. Anafanana kila siku, kila sehemu.
Viongozi wa dini wa awamu hii wametekwa na kikundi fulani cha wana siasa ambao wao kwao ni mwendo wa kupanda madhabahuni kuhubiri huku mambo lukuki yakiwa yamejificha ndani ya mioyo yao.