Uchaguzi 2020 Ninamshauri Dkt. Magufuli aache kusema alivyofanya na aseme atakavyofanya akichaguliwa tena

Uchaguzi 2020 Ninamshauri Dkt. Magufuli aache kusema alivyofanya na aseme atakavyofanya akichaguliwa tena

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Wanaukumbi kwanza niseme wazi kuwa mimi ni Mwanaccm kindakindaki na nyuzi zangu humu zinafahamika tangu nimejiunga na chama hiki miongo kadhaa iliyopita

Kwa miaka mitano kila television, magazeti na vyombo vingi vya nje na ndani ya nchi vimeeleza mambo muhimu aliyoyafanya rais Magufuli ikatosha , kwa sasa tunafanya kampeni na wenzetu wananadi sera hivyo sera hushindana na sera na sio kila mtu anazipata na kuzisoma ilani za vyama wengi tunategemea kusikia majukwaani tu.

Tabia ya Watanzania wengi sio kusoma ni kusikia na hizi ilani hazisambazwi sana kwa jamii hivyo kuna haja ya mgombea wetu kuisemea sana tena sana zaidi ya hapa

Kila Mtanzania anafahamu kuwa Rais Magufuli kafanya nini ktk kipindi cha miaka mitano, he is excellent for the maxim so sio habari tena inabaki kuwa legacy kama atamaliza muda wake na hapa tuelewane ubora wa kiongozi unapimwa kwa anavyomalizia utawala wake sio anavyoanza na huu ndio mtihani kwa watawala wengi maana wengi huharibu mwishoni .

Watu wanataka atafanya nini kipya kama atachaguliwa tena na wameelekeza mawazo yao kwenye ajira, mikopo, fao la kujitoa, ongezekeo la mishahara na n.k

Mambo ya ujenzi yameimbwa sana ndani ya miaka 5 na sio habari tena kama tunavyosema katika tasnia ya habari kuwa kama inafahamika ifahamishwe ya nini ?

Please jopo la kampeni mwambieni JPM aseme atafanya nini sio alifanya nini?

USSR
 
Wewe unafuatilia kampeni za JPM? Husikii ahadi za nini atafanya? Husikii habari za kununua ndege zingine tano na kukamilisha Sgr,we bwege sana.
Kwani ninyi hamjuani?
Huyu ni mwenzenu Ametoa ushauri mzuri Ameona kuna kasoro kwenye kampeni za mkulu
Ilikuwa vyema ungezingatia ushauri huu kuliko kumtukana though it's too late
Ninyi ndio mnaomdanganya mnufaike ninyi na familia zenu
Ficha ujinga wako walau kwa sekunde chache
Deal na reality bro bra bru kha
 
Wanaukumbi kwanza niseme wazi kuwa mimi ni mwanaccm kindakindaki na nyuzi zangu humu zinafahamika tangu nimejiunga na chama hiki miongo kadhaa iliyopita...
Ashasema anataka Sugu amsugue, ataoa mke mwingine zenji, atanunua ndege 5, atajenga uwanja mkubwa wa mpira Dodoma na mengine mengi tu we unataka nini tena halafu kama kweli upo kwenye chama chetu haya unayoongea hapa si ungeyaleta kwenye chama sasa why unayaleta mitandaoni?? we chadema nini??

halaf Samia ashasema hata wakipiga kura kule kwengine ccm ndiyo itakayounda serikali, na ashasema kurudi kwa wananchi kuomba kura ni hisani tu kwani chama kikongwe kama ccm wala hakukuwa na haja ya kuomba kura wala kampeni maana tutashinda kwa asilimia trilioni trilioni.
 
Ashasema anataka Sugu amsugue, ataoa mke mwingine zenji, atanunua ndege 5, atajenga uwanja mkubwa wa mpira dodoma na mengine mengi tu we unataka nini tena halafu kama kweli upo kwenye chama chetu haya unayoongea hapa si ungeyaleta kwenye chama sasa why unayaleta mitandaoni?? we chadema nini?? halaf Samia ashasema hata wakipiga kura kule kwengine ccm ndiyo itakayounda serikali, na ashasema kurudi kwa wananchi kuomba kura ni hisani tu kwani chama kikongwe kama ccm wala hakukuwa na haja ya kuomba kura wala kampeni maana tutashinda kwa asilimia trilioni trilioni.
Ccm ina ilani yake ya 2020-2025. Hizo ndizo ahadi za nini kitafanyika.
 
Back
Top Bottom