Kwenye kampeni kwanza unatoa ripoti ya ulichofanya kwa wapiga kura
lazima utoe ripoti kwao.Ulienda na ilani ukasema nitafanya hivi sasa ni je ulifanya?
Ukishamaliza kutoa ripoti ndio sasa unaingia kuwaeleza mapya yepi utafanya kwa walio wengi ambayo tayari yapo kwenye ilani ya chama ya 2020-2025.
Ilani hujikita hasa sio kwa walio wachache bali walio wengi ndio maana utakuta inabeba mambo mazito ya kuwasaidia walio wengi katika jamii kwanza kama miradi mikubwa ya maji,umeme,mabarabara nk yanayofaidisha umati wa walio wengi katika jamii kisha ndipo una address ya walio wachache sio kinyume chake.Huanzi na ya walio wachache halafu unamalizia ya walio wengi
Mapya ya CCM Yako kwenye ilani
Kutoa ripoti kwa yale yaliyokwisha fanywa ni lazima kwa kila mgombea awe mgombea uraisi,ubunge au udiwani aeleze kilichofanyika kwanza ndio aendelee kueleza kitakachofanyika.Wananchi lazima wapewe mrejesho ndio maana wabunge wa upinzani wanapata shida sababu hawana ripoti ya mrejesho ya walichofanya wanaishi kwa ahadi hewa tu kila mwaka zisizo na ripoti ya walichofanya
CCM hatuwezi waiga wao