Ninani basi aliyewaambia wabongo pilau lazima ipikwe siku ya sikukuu?

Tena kupangiana mkuu
 
Japo wengi mnatamani, ila humo kuna mate, kamasi, nyewle, vinyesi, n,k kiwe kimeandaliwa nyumbani au kwenye restaurant, n.k.

Sisi wabongo ni wachafu sana na hatuna kinyaa japo kimavazi unaweza kuona ni wasafi.

Mtanisamehe.
Sijakuelewa mkuu
 
Pilau linahutaji maandalizi mengi kidogo tofauti na wali, pia pilau mwenzake nyama.
Unaposema pilau linatofautian na wali mweupe kwa buku 2 sio kweli jombaa

Pilau la sikukuu lina vikorombwezo vingi ambavyo kuviandaa kwa siku ya kawaida inakubidi utenge muda mwingi kwa kazi hiyo tu.
 
Siyo kweli. ukiingia ndani saana haya ni mautundu tu ya upishi mkuu hayo makolobwezo uyasemayo ni utundu tu.

Hata wali wapo wanaopika kwa mbwembwe mno hadi unaogopa yaani utofauti inakuwa ile rangi tu (palau masala )

kama ukibisha tuweke mahitaji hapa ya pilau na wali hapa nami ni mpishi kwa level yangu najua abc
 
Vikorombwezo vinavyoendana na pilau kama kachumbari, chachandu, juice /soda ndivyo nilivyomaanisha
 
Sikukaribishi tena kwangu, kumbe ulikuwa unapiga picha pilau letu. Yote haya ni majanga ya CCM.
 
Vikorombwezo vinavyoendana na pilau kama kachumbari, chachandu, juice /soda ndivyo nilivyomaanisha
Hivyo ni ziada tu hata jkwenye wali unaweza weka mkuu. kifupi mapishi yanatofautiana sana kati mtu na mtu na jamii hii kwa jamii nyingine. wee angalia samaki anavyopikwa na wachina niliwahi ona clip moja viungo zaidi ya 17 kwenye mboga moja nayo ni samaki ....wale jamaa hapana wanaweka hadi na magome ya miti,mizizi na majani bado viungo vya kimiminika asee mchuzi unakuwa mweusi kama mkaa
 
Hoja imekubalika
 
Mi naongelea kikwetu kwetu mkuu , familia zetu hatuweki vikorombwezo vingi kwenye vyakula vya kila siku ila inapofika sikukuu sasa ndio vile vyote wanaweka sasa.

Mtu katoka job kachoka aanze kuandaa kachumbari, sijui chachandu atengeneze juice wakati anaweza tia mchele kwenye rice cooker akasubiri wali chap.
 
Kaka Kuna watu wanatatizo la mdomo kutofunga Sasa kwa picha hizi tegemea kuona wamekomenti maneno yasyoeleweka maana mate yatajaa kwenye screen za simu zao
 
Pilau ikipikwa kila siku itapungua ule uthamani wake na umuhimu wake,itaonekana ni chakula cha kawaida tu,Sikukuu lazima kuwe na vitu special,

Ndio maana hata watoto huvaa nguo mpya,na wanajua kua siku ya sikukuu lazima wavae nguo mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…