Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Inawezekana anapitia changamoto kweli ila ameshindwa kufunguka kwenye Kila eneo, kwa maana asingesema atafutiwe kazi kwakua anayo hiyo diploma ya ualimu kama asingekua nayo kweli.

Logic yako unaijenga kupitia UDSM lakini this is jamiiforum so watu hupenda kutoa taarifa kwa codes, ndio maana taarifa nyingi za humu hiko sahihi kwa asilimia 100 kwenye eneo la ujumbe unaotakiwa kufikishwa ila maeneo na takwimu nyingi huwa ni za picha.

Kwenye hili bandiko la huyu ndugu yetu kuna ukakasi katika maeneo hayo mawili, ya cheti hadi kwenye diploma na hapo kwenye huyo mdogo wake wa kidato cha tatu. (Kuna uwezekano huyo anaemuita mdogo wake akawa ni mwanae au akawa ni kweli anae mdogo wake ambae anahitaji msaada ila hayupo kidato cha tatu kama alivyo sema)

So kwakua Miss Natafutwa mlengo wa bandiko lako ni kutaka kutiwa moyo na uwezekano wa kusaidiwa basi ungejaribu kuweka sawa hayo maeneo kwa kutoa maelezo ya kina ili kulifanya hili bandiko lako liwe na mlengo mmoja kuliko kuwa na mijadala miwili yenye mlengo tofauti kama hivi sasa.
 
Pole sana Mama. Kuna mdau hapo juu kaishatoa msaada kwa mdogo wako.

Sasa turudi kwako.

Kama utaona inafaa, uza hiyo nyumba uliyojenga. Unaweza pata fedha nzuri. Nenda Mbeya au songwe. Maisha kule ni rahisi.

Tafuta kiwanja cha bei rahisi, Unaweza jenga chumba na sebule chap. Huku ukiwa umepanga, vyumba ni bei rahisi Sana.

Tafuta kazi kwenye zile kampuni za usafi wa maofisini (Huwa wanahitaji sana watu) huku unatafuta dili la kufundisha ( Mbeya mjini kuna tuition centres nyingi sana ). With time utapata.

Wakati hayo yanaendelea anza kutafuta fursa za kilimo cha kununua mazao upande wa Songwe hasa Mpunga na Mahindi, Ukifanikiwa unakuwa unauza gunia moja moja kwa kuingia mkataba na watu wa Mashine za kusaga na kukoboa.

Mwisho.

Jiepushe na watu wanaokatisha tamaa, usiwaze Sana wala usikate tamaa Kila mtu anapitia changamoto zake zinazoweza kuwa nzito zaidi ya zako.

Mshukuru sana Mungu huna changamoto yoyote ya kiafya na huo ndio mtaji wako Mkubwa saaaana.

Usikubali kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kirahisi tafadhali Sana ( Hata kama akitokea mwanaume hapa wa kukusaidia, jitahidi sana uchore mstari wa msaada au mawazo ya kujenga tu na usije ingia kwenye Mapenzi) angalau mpaka uhakikishe una uwezo wa kujitunza wewe na mtoto. Kwa sababu ukipata mimba na mtoto sasa hivi Mambo yanaweza kuwa magumu zaidi.

Mungu akutunze na akubariki Sana Mpendwa.

Asante.
 
pole ila kama cheti kilichomwa moto unaeza enda pale NECTA siku hizi wanautaratibu wa kusaidia waliopoteza vyeti wanapewa vingine
 
Mmh pole inasikitisha sana. Hongera Kwa kujitambua ila Sasa afya yako Kwa hiyo miaka 6 ilinusurika kwel?
 
Amina Manyanza ....yaani sihitaji kabisa kurudi nilikotoka.
Na wala sitaki kukumbuka maisha yangu ya nyuma.
Hat ushauri wenu pia unanipa moyo mno.
Nawashukuru sana.
Vumila tu maana kila siku mambo huwa yanabalika endelea kuwa na tumaini tu. Mambo yatakaa sawa. Endelea kutafuta kitu kitakachoamua kupatia kipato hata kama ni kidogo kutosheleza maisha yako ya kila siku.

Halafu ondoa ile hali ya kuyakumbuka maisha ya udada poa maana Dada poa huwa wanaishi maisha ya maigizo na magumu sana. Ishi maisha yako halisi.
 
PGDE.
Ni mdogo wangu na si mwanangu.
Cha umuhimu ni kuwa nahitaji ajira na uhitaji.
Kama unaweza kunisaidia sawa ila kama utaona haikupendezi basi usinizibie riziki kwa wanaotaka kunisaidia.
Ulitumia cheti cha kidato cha nne kusomea Post Graduate Diploma? Acha upumbavu aisee. Mods futeni huu uzi wa huyu TAPELI.
 
Akacheze na wenzie huko kuna sehemu kajichanganya ina maana anayoyasema sio ya kweli ni anatunga tu kasahau kuandaa vizuri maelezo.

Kama story ingekuwa ya kweli ingekuwa na mtiririko ulionyooka vizuri. Hata hivyo pia kama anatafuta kazi angeandika tu natafuta kazi ninasomesha pia nina hali mbaya ya ki uchumi
 
Mkuu Miss Natafutwa pole Sana ndugu yangu ,hakika dunia duara .
Sina msaada kwa vyote ulivyohitaji katika maombi yako Ila najihisi kufanya lolote ili uondokane na hiyo Hali
Naomba tuwasiliane 😭😭
 
Post Graduate Diploma?

Unazidi kujichanganya Mkuu.

Mimi sikuzibii riziki, ila najaribu kukudadisi ili kuweka msawazo.

Maelezo yako yana ualakini mwingi.
HUYU NI TAPELI. Ninakerwa na matapeli ila ninakerwa zaidi na matapeli yasiyo na akili kama huyu Miss Natafutwa ... cheti cha form 4 ukasomee PGD si maajabu ya karne?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…