Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Inawezekana anapitia changamoto kweli ila ameshindwa kufunguka kwenye Kila eneo, kwa maana asingesema atafutiwe kazi kwakua anayo hiyo diploma ya ualimu kama asingekua nayo kweli.Mleta uzi ni tapeli asiye na akili.
Ili uwe tapeli tena wa kuwatapeli wanaJF, basi uwe guru katika kutengeza uongo unaoendana na ukweli kwa zaidi ya 90%. Basi hata uchukue hela zao ila ukitumia akili nyingi katika strategy zako.
Haiwezekani abadani ukasoma UDSM Diploma.
Nimeuliza anasema eti ni PGD.
Post Graduate bila Degree? Ama bila Advanced Diploma? Aisee!.
Anachodai alitumia cheti cha mtu kwa sababu chake kiliteketea, hii inamake sense kwa wapuuzi wenzake tu.
Anadai wazazi wake walimuacha na mdogo wake. Huku gap yake yeye na mdogo wake wa KIPEKEE ni zaidi ya miaka 25, hii inakuingia akilini? Kama ndiyo, basi wewe ni mpuuzi pia.
Mtoa mada, anatumia sensitiveness ya swala la kujiuza. Kuwa idadi kubwa ya wanajamii hawawezi na kamwe wasingetaka mtu aliyeacha kujiuza ila arudi huko. Hivyo, anataka huruma ya jamii juu yake.
Huu ni ukuda. Upumbavu wa ajabu.
Logic yako unaijenga kupitia UDSM lakini this is jamiiforum so watu hupenda kutoa taarifa kwa codes, ndio maana taarifa nyingi za humu hiko sahihi kwa asilimia 100 kwenye eneo la ujumbe unaotakiwa kufikishwa ila maeneo na takwimu nyingi huwa ni za picha.
Kwenye hili bandiko la huyu ndugu yetu kuna ukakasi katika maeneo hayo mawili, ya cheti hadi kwenye diploma na hapo kwenye huyo mdogo wake wa kidato cha tatu. (Kuna uwezekano huyo anaemuita mdogo wake akawa ni mwanae au akawa ni kweli anae mdogo wake ambae anahitaji msaada ila hayupo kidato cha tatu kama alivyo sema)
So kwakua Miss Natafutwa mlengo wa bandiko lako ni kutaka kutiwa moyo na uwezekano wa kusaidiwa basi ungejaribu kuweka sawa hayo maeneo kwa kutoa maelezo ya kina ili kulifanya hili bandiko lako liwe na mlengo mmoja kuliko kuwa na mijadala miwili yenye mlengo tofauti kama hivi sasa.