Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Usiwe mwepesi wa kuhukumu bado Kuna baadhi ya maelezo yanaeleweka vizuri, mpe moyo maisha yanabadilika.
 
Naamini ulivyo andika juu ya Kaka Max

Ukienda ofisini kwake aka kuona na kutoa taarifa hapa bila kukutana au kuweka picha yako kama hautaki

Basi mdogo wako atapataja pesa za kusomeshwa na Mahitaji mengine kama yeye

Taja shule anasoma na Mahitaji watu wanunue apewe

Ila hakuna ada si ndio so hayo mengineyo

If unataka kweli naamini ukiwa umesema umatafufa kazi nawe utakuwa unajiongeza kivyako
 
Dada acha haya majadiliano, unaanza kunikwaza; endelea na mengine niweze kuendelea kukusitiri!
Utttoh unataka kumsaidia kusoma jambo zuri sana. Je kama hataki...angalia historia ya elimu yake na miaka yake hapo anaweza asiwepo rahisi sana kusoma. Vilevile ktk suala la elimu yake na wewe unataka kumpeleka kusoma hoping degree kma ni ya TCU huwa Wana link data za NECTA Sasa huyu atapita kweli hapo na anacheti fake.l Cha PDGE aliyoipata kwa cheti Cha form four tena fake. Kwanza PDGE ni post graduate ktk elimu. Sasa alifikaje kuwa graduate na kwenda kusomea elimu. Maana yake huyu ana degree nyingine au diploma nyingine isiyokuwa ya elimu. Sasa sula la vyeti fake linatoa ukakasi. Application zote za vyuo zinapitia kwa TCU kwa ku link form four index number. Anyway, elimu yake inanukakasi. Ni bora kuomba msaada au kutoa msaada bila kuzingatia details. Kuna details ametoa hazilink up.
 
Pole na changamoto unayopitia...

Huyo mdogo wako anasoma Shule za binafsi (Kulipia) ama Shule za Serikali?

Tukijua mahitaji yake ya kusoma kwasasa, na tukathibitisha, tunaweza kumchangia japo yeye aendelee na masomo

Umesema uliondolewa Kazini kutokana na ile skendo ya Vyeti feki, Rudi Kwa mwajiri wako wa zamani (Halmashauri) wakupe barua ya kukufukuza kazi kisha uitumie kwenda kwenye Taasisi uliyokuwa unachangia pension ili wakupe fao la kukosa ajira ili walau liku-boost wakati huu mgumu unaopitia.

Mungu akupe uvumilivu ili usije kufanya maamuzi ambayo yanaweza kukutengenisha naye.

Kila la heri Mkuu
 
Umeongea ukweli ambao pia kwa namna fulani ni kama umetubu uliyowahi kuyafanya. Nakupa pole kwa uliyoyapitia na hata sasa unayopitia.
 
Pope sana dada, Natumai wenye uhitaji wata kusikia.

Mzee wangu Ushimen, Shimba ya Buyenze, Grahams, Mshana Jr msikilizeni dada yetu hapa
Nimeona andiko lake, Kuna vitu nimeshauri kupitia maoni niliyoyatoa hapo juu,

Kama ataweza atuletee uthibisho wa nyaraka ili tuweze kumchangia ili mdogo wake aendelee na masomo.

Na Kwa kuwa JF ni pool kubwa, natumai wenye uwezo wa kumwajiri watafanya hivyo

Najua Kuna baadhi yetu humu ndani, tunafanya biashara ya Shule(tunamiliki) kwahiyo ni rahisi wakiona ana sifa hasa ya uzoefu wampe ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…