Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Huu ni uongo.

Kwanza, kinachomata haswa ni index number ya kidato cha nne. Cheti huwa ni nyongeza tu baadae, hapa nazungumzia katika mchakato wa kuomba vyuo, nk.

Lakini pia, ukichoma cheti ama kukipoteza kwa bahati mbaya, utaratibu upo very clear. Omba loss report, andika barua kwenda NECTA, watakutengenezea cheti kingine.

Kudai ulitumia cheti cha mtu kwa sababu chako ulichoma ni upuuzi usio na mantiki.
Cheti huwa ni kimoja tu hawatoi cha pili, huo utaratibu iliouweka utakusaidia kupata statement of results only ambayo itakusaidia kuendeleq na elimu au kupata kazi
 
Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.

Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.

Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.

Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza). Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini. Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.

1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu), Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.

Asanteni.
Pole sana!! Kuna nafasi ya kuuza duka la spear za pik pik Kahama, utakuwa tayari?
 
Min tangazo limeeleweka, huyo mtoa post km ana shida ya kazi kulikuwa na umuhimu gani wa kusema km aliwahi kujiuza??

Hivi unaweza kuomba kazi ya ulinzi halafu ukasema uliwahi kuwa mwizi?? Akili kumkichwa
Kwamba anaomba kazi ya kulinda vibunda ila kwenye cv kuna sifa ya wizi🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom