Ninapoishi ni mimi pekee ambae sijaoa

Ninapoishi ni mimi pekee ambae sijaoa

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,236
Reaction score
7,583
Habari wakuu, (Brothers, Sisters, Baba na Mama mliomo humu)
Kama heading inavyosema hapo juu, Ni kwamba nilipopanga chumba nimejikuta mimi pekee ndiye sina mke, Ipo hivi;

Mimi ni kijana mwenye miaka 23 na niliwahi kuishi na mwanamke (yeah, niliishi na dada mmoja tuliishi kwa miaka mitatu na mwaka jana ndo tulifikia tamati kutokana na mmoja wetu kwenda kinyume na makubaliano yetu tukaachana) ambao walifuatiliaaga kisa changu cha mwaka jana kwenye miezi kama hii nilieleza ni kwa jinsi gani alivyonikatili moyo hadi kufikia kuachana)

So now ni mwaka sasa umepita nipo single na nimekuja kushtukia vijana wenzangu wote (majirani) wanaishi na wapenzi wao (sio kwa ndoa ila wanaishi kama mume na mke), Hapa ninapoishi tupo wapangaji 6 na asilimia kubwa wote ni vijana sasa nimejikuta napata aibu kwa kuwa wenzangu wote wanaishi na wenza wao.

Nahisi aibu ninapoishia kununua percel kwaajili ya kula wakati wenzangu wanapikiwa na wake zao, Wanafuliwa ila mimi nafua mwenyewe, Wanalala wamekumbatiana mimi nalala peke yangu kama nimetengwa.

Though wanajua sababu na wanafahamu kwamba nilishaishi na mwanamke ila tukaachana maana ninapoishi bado ni palepale nilipokuwa nikiishi na yule Ex wangu ila nimeanza kujihisi labda sipaswi kuishi hapa tena maana ni kama naaribu mpangilio sahihi walionao wenzangu maana hata mpango wa kuoa bado sina kwa sasa.

Ubaya sio kwamba na mimi nashindwa kuwa na mtu wa kuishi nae ila ni kwamba baada ya kuachana na yule dada nimejikuta nikiyachukia mahusiano kabisa na kuona kwamba maybe kwa sasa sipaswi kuwa na mtu na labda ninatakiwa kufocus kutafuta maisha pekee kwa sasa na to be honest ni kwamba na-enjoy kinoma kuishi mwenyewe ila sasa haya mazingira ninayoishi ndo yanafanya nione aibu na kujiuliza kwamba wenzangu wananichukuliaje mimi kuishi peke yangu na wao wote wanaishi na wenzao.

Je, una cha kunishauri? Na je, Ulishawahi kuishi mazingira kama yangu? uliwezaje ku-handle?
 
Sema uliwahi sana, yaani una 19-20 years unaishi na mwanamke? Yeye alikua na umri zaidi yako au pungufu? Sio case ni past.

Ushauri:
1. Kula sana maisha. Party sana. Watafune sana. Club Disco Outings za kutosha. Hadi ufike 25/26 ndio stay na mmoja.

2. Hao mademu unaowapata sahivi usiwalete kwako. Heshimu ghetto lako mmalizane uko uko loji.

3. Usiogope wenzako wanakuchukuliaje. Wenyewe wanatamani wawe kama wewe. Trust me.

4. Usiwe unashinda sana home usije jenga mazoea na wake za watu. Waume zao watakuhisi vibaya ata kama ni mazoea ya: Mambo vipi, naazima pasi, karibu tule.

5. Shinda jukwaa la "Love Connect" kuna wadada wazuri wanatafuta wapenzi wadogo wadogo kama wewe. Ila kuna majina nitakuPM usiwaguse. Wa sisi kaka zako.
 
Ishi utakavyo na siyo watakavyo, unaweza kudhani hao wanaoishi na wenza wao wanaenjoy kumbe wapo jehanamu ya duniani, hakuna jina la sweet wala honey humo ndani, ni mbwa wewe, Ng'ombe wewe, pumbavu wewe.

Naona umechoka kuishi kwa raha unatamani kurudi utumwani.
 
Maisha yako usiyafananishe na ya mtu wala ya mtu usijifananishe nayo, ishi vile ulivyo utakua na amani sana.

Wakati mwingine wao wanatamani wangekuwa kama wewe wakati wewe unatamani ungekuwa kama wao.
 
Jinga wewe, ongea kwa umoja bana[emoji23]
Sema ukisahi sana, yaani una 19-20 years unaishi na mwanamke? Yeye alikua na umri zaidi yako au pungufu? Sio case ni past.

Ushauri:
1. Kula sana maisha. Party sana. Watafune sana. Club Disco Outings za kutosha. Hadi ufike 25/26 ndio stay na mmoja.

2. Hao mademu unaowapata sahivi usiwalete kwako. Heshimu ghetto lako mmalizane uko uko loji.

3. Usiogope wenzako wanakuchukuliaje. Wenyewe wanatamani wawe kama wewe. Trust me.

4. Usiwe unashinda sana home usije jenga mazoea na wake za watu. Waume zao watakuhisi vibaya ata kama ni mazoea ya: Mambo vipi, naazima pasi, karibu tule.

5. Shinda jukwaa la "Love Connect" kuna wadada wazuri wanatafuta wapenzi wadogo wadogo kama wewe. Ila kuna majina nitakuPM usiwaguse. Wa sisi kaka zako.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umenichekesha mwishoni ila shukran mkuu🙏
 
Ishi utakavyo na siyo watakavyo, unaweza kudhani hao wanaoishi na wenza wao wanaenjoy kumbe wapo jehanamu ya duniani, hakuna jina la sweet wala honey humo ndani, ni mbwa wewe, Ng'ombe wewe, pumbavu wewe.

Naona umechoka kuishi kwa raha unatamani kurudi utumwani.
Hapana mkuu sitamani, ila ni mazingira tu kama ndo yanataka hivyo
 
Back
Top Bottom