Ninapoishi ni mimi pekee ambae sijaoa

Ninapoishi ni mimi pekee ambae sijaoa

Habari wakuu, (Brothers,Sisters, Baba na Mama mliomo humu)
Kama heading inavyosema hapo juu, Ni kwamba nilipopanga chumba nimejikuta mimi pekee ndiye sina mke, Ipo hivi;

Mimi ni kijana mwenye miaka 23 na niliwahi kuishi na mwanamke (yeah, niliishi na dada mmoja tuliishi kwa miaka mitatu na mwaka jana ndo tulifikia tamati kutokana na mmoja wetu kwenda kinyume na makubaliano yetu tukaachana) ambao walifuatiliaaga kisa changu cha mwaka jana kwenye miezi kama hii nilieleza ni kwa jinsi gani alivyonikatili moyo hadi kufikia kuachana)

So now ni mwaka sasa umepita nipo single na nimekuja kushtukia vijana wenzangu wote (majirani) wanaishi na wapenzi wao (sio kwa ndoa ila wanaishi kama mume na mke), Hapa ninapoishi tupo wapangaji 6 na asilimia kubwa wote ni vijana sasa nimejikuta napata aibu kwa kuwa wenzangu wote wanaishi na wenza wao, Nahisi aibu ninapoishia kununua percel kwaajili ya kula wakati wenzangu wanapikiwa na wake zao, Wanafuliwa ila mimi nafua mwenyewe, Wanalala wamekumbatiana mimi nalala peke yangu kama nimetengwa... Though wanajua sababu na wanafahamu kwamba nilishaishi na mwanamke ila tukaachana maana ninapoishi bado ni palepale nilipokuwa nikiishi na yule Ex wangu ila nimeanza kujihisi labda sipaswi kuishi hapa tena maana ni kama naaribu mpangilio sahihi walionao wenzangu maana hata mpango wa kuoa bado sina kwa sasa.

Ubaya sio kwamba na mimi nashindwa kuwa na mtu wa kuishi nae ila ni kwamba baada ya kuachana na yule dada nimejikuta nikiyachukia mahusiano kabisa na kuona kwamba maybe kwa sasa sipaswi kuwa na mtu na labda ninatakiwa kufocus kutafuta maisha pekee kwa sasa na to be honest ni kwamba na-enjoy kinoma kuishi mwenyewe ila sasa haya mazingira ninayoishi ndo yanafanya nione aibu na kujiuliza kwamba wenzangu wananichukuliaje mimi kuishi peke yangu na wao wote wanaishi na wenzao.

Je, una cha kunishauri? Na je, Ulishawahi kuishi mazingira kama yangu? uliwezaje ku-handle?
Oa kijana usijevamiwa na pepo la kuvizia wake za watu watakaosafiri safari za mbali.
ukaanza kusaidia kutunza familia isiyokuhusu,na hata ukibahatika,kumpa mimba
huyo mama hutakuwa na guts za kusema huyo atakayezaliwani mwanao japo utakuwa unatumwa udongo ,maembe mabichi na limao.
 
Dogo nakuangalia kwa jicho la mbali nakuona unataka kuanza kuwaka tamaa kwa wake wa wenzio, acha hiyo kitu ya ujinga wewe kuanzia leo ni kuingiza pisi na kutoa uwe na vipimo vikubwa vya kutosha tu furahia maisha yako na utapata mitego mingi sana kutoka kwa hizo mke za wenzako vumilia,usiingie ni mtego mkubwa sawa wa kuliwa kiboga ukiwa mdogo.!
 
dogo nakuangalia kwa jicho la mbali nakuona unataka kuanza kuwaka tamaa kwa wake wa wenzio, acha hiyo kitu ya ujinga wewe kuanzia leo ni kuingiza pisi na kutoa uwe na vipimo vikubwa vya kutosha tu furahia maisha yako na utapata mitego mingi sana kutoka kwa hizo mke za wenzako vumilia,usiingie ni mtego mkubwa sawa wa kuliwa kiboga ukiwa mdogo.!
sawa mkuu🤝
 
Back
Top Bottom