Ninapokuwa na Mawazo, chupa ya maji inageuka bia

Ninapokuwa na Mawazo, chupa ya maji inageuka bia

The ghost writer

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2023
Posts
967
Reaction score
1,971
Kama ilivyo kwa binadamu wenzangu wengine Kuna wakati napitia msongo mkali wa kimawazo nakuwa na hamu sana ya kunywa bia kwa lengo la kujisahaulisha na shida. Ila nikifiria madhara yake hasa magonjwa ya Figo, kufilisika matatizo, kugombana na ndugu, wazazi, mke n.k naamua kutafuta tu hobbies nyingine zitakazonirudishia mood (Hali yangu ya kawaida)

Moja ya hobbies hizo ni kunywa maji. Mawazo yakinishika nakunywa sana maji. Nitanunua chupa nyingi za maji nayanywa kama wengine wanavyokunywa pombe nikiona haotoshi nayawekea limao basi maji yanakuwa machungu. Ule uchungu wanaouhisi wengine wakinywa pombe nami nafeel kiwango sawa kabisa ninapokunywa maji ya limao. Hapo nitakunywa hata chupa kumi za maji ya Litre 1 kwa siku.

Hio ndio pombe yangu. Japo changamoto zake ni usumbufu wa kwenda kukojoa, but that thing make me feel better
 
Back
Top Bottom