John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 379
- 1,412
Unaponunua umeme unakatwa Kodi ya Ongezeko la Thamani ambayo ni Asilimia 18 ya pesa uliyotoa, kisha TANESCO wanakukata 1% wanasema ni hela ya EWURA, baada ya hapo . TENA unakatwa 3% eti pesa ya REA.
Je, kwa nini mlaji anaigharimikia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA)? Hapo bado kuna makato ya pango ambayo yanakatwa mara moja kwa mwezi.
Hizi si ni mamlaka za Serikali? Kwa nini zimlemee mtumiaji wa umeme? Kodi ya Ongezeko la Thamani si ingetosha?
Mbona Polisi, DAWASA, BANDARI na wengine hatuwalipii?
Kuna maswali kadhaa ambayo natamani Serikali ingetupatia majibu yake:
1. Nani aliwapa mamlaka TANESCO ya kukata 1% ya tozo kwa ajili ya EWURA? Wanao waraka wowote unaowaelekeza kukata hiyo pesa?
2. Wakiikata wanaipeleka wapi na kwa ushahidi gani? Wanawapa EWURA au wanapeleka HAZINA?
3. EWURA kama mamlaka nyingine yoyote ya serikali haipati bajeti yake toka serikalini ambayo inatokana na ile 18% VAT tunayolipa ? Kwa nini tena iwatoze watumia umeme tozo ya ziada?
REA ni mamlaka ya Serikali chini ya TANESCO inayohusika na kuwapelekea Wananchi Vijijini umeme kwa bei nafuu, kwa ruzuku ya Serikali.
Kwanini TANESCO wanatukata 3% kila mtumiaji wa umeme ili kuipeleka REA?
Kwani chanzo cha fedha REA ni wapi? Kama REA ni kampuni tanzu ya TANESCO kwanini wanawakata pesa wanunuzi wa umeme kwa ajili ya uendeshaji wa shirika lao? Kwanini pesa hii wasitozwe hao waliopatiwa umeme kwa bei ya ruzuku peke yao?
Mimi ambaye sikupata umeme kwa njia ya ruzuku kwa nini nabebeshwa mzigo wa kumlipia mwingine?
Gharama za uendeshaji wa REA hazitokani na kodi za Serikali? Kunikata VAT na kisha 3% ya REA sio kulinipisha kodi mara mbili kwa kitu kilekile?
Pia soma ~ LUKU - VAT 18% + EWURA 1% + REA 3% = 22%. i.e. 22% of the money you want to buy electricity is tax