John Gregory
JF-Expert Member
- Jul 14, 2019
- 1,137
- 2,147
Mara nyingi huwa ninaona watu wakijaribu kulinganisha vilabu hivi viwili vya Yanga na Simba, Ila kiuhalisia vilabu hivi vinatofautiana sana kiumri,mafanikio na hata kihistoria.
1.Kiumri Yanga ilianzishwa February 11, 1935, Mwaka mmoja kabla ya kuanzishwa Simba Sc, kwa hiyo kiumri ni wazi Yanga Sc ni kaka yake na Simba Sc.
2.Kimafanikio ndani ya nchi, Yanga ndiye timu iliyowahi kutwaa vikombe vingi zaidi katika Ligi kuu bara (kiambatanisho), Pia Yanga Sc imetwaa mataji mengi zaidi ya Simba Sc katika mashindano mengine ya ndani ikiwemo FA Cup na Ngao ya jamii.Kwa takwimu hizi nitashangaa kuona mtu akilinganisha Yanga Sc na vilabu vingine hususan ndani ya nchi.
3.Kimafanikio nje ya nchi, Yanga sc ndiye timu pekee iliyowahi kushiriki nusu fainali na hatimaye fainali na endapo itatwaa kombe basi itakuwa club ya kwanza kutoka Tanzania kushiriki na hatimaye kutwaa taji la moja ya mashindano makubwa zaidi ya mpira wa miguu barani Afrika.
Kwa mafanikio na historia hii ya Yanga sc, Nitashangaa sana kuona club hii ikilinganishwa na timu yoyote ndani ya Tanzania.