permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
Hii ya kila aya kumalizia "mbele ya hao wanaume" kunatoa picha ya aina yake.Yes shirikisho ni kombe rahis mno yeyote anaweza kubeba kulingana na upepo upepo umemwangukia vipi ,ni kombe ambalo huwez kutabir Nan anatwaa tofaut na club bingwa unaweza kutabir kabisa kuwa kati ya Alhly ,mamelod ,raja au wydad mmoja wapo atabeba .
Sasa embu niambie huko shirikisho ni timu zipi unaweza kuzitabilia ubingwa?
Mwaka Jana Berkane kabeba hilo kombe vipi huu msimu kaishia wap?
Hapa hakuna kukwepa ukweli kipimo sahihi Cha timu yeyote Ile ndani ya hili bara ni huko club bingwa ,ukipasua huko hayo ndio mafanikio ya maana na utaanza kujiamin mbele ya wanaume.
Pesa anayopata mshindi wa pili shirikisho ni sawa na pesa anayopata mtu aliyeishia robo club bingwa, Bado huon huo utofaut.
Yanga wamejitahid hatukatai ila swala la kujimwambafai et mnamzid Simba kimataifa huko ni kukosa heshima .
Wasudan tu na waganda wamewatoa jasho je ungeweza kupenya Kwa hao wanaume?
Hayo anayofanya mayele mbele ya marumo angeweza kutakata mbele ya mamelod ,Alhly ,raja ,wydad,Esparance ,Simba,Petro de Luanda?
Kama yanga ni kubwa Kwa Simba basi msimu ujao tunataka yanga athibitishe hilo angalau Kwa kufika hata robo club bingwa alafu baadae ndio tukae tuongee kuwa yanga ni mkubwa Kwa simba
Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app