Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Nina mikopo nilichukua 2018 unaisha 2030
Sijawahi jutia kwasababu niliupeleka kwenye biashara na biashara inatembea.

Usikope ukaanze biashara, kopa ukaendeleze biashara.

#YNWA
 
Mkuu, kama mpambanaji nakushauri uchukue huo mkopo,
Ukiwekeza kwenye biashara ya kukupa 10% per month ina maana utakuwa unatengeneza 5M kisha unawapa bank 1M yao wew unabaki na 4M,

Kikubwa fikiria biashara hio vizuri, najua mpaka kuwa na access ya kukopa 50M wew sio mtu mdogo, ila pia kama kuna chance ongea na koan officer washushe riba kidogo,
Kama atakaza wew beba huo mkopo,

Unaweza usikope kuhofia hio 40M ila miaka 9 itaisha na utajikuta huna hio 50M wala hio 40M ya bank
 
Mkuu kwa ushauri.tu, nenda na NMB ukalinganishe. Hiyo riba crdb na marejesho ni kubwa mno.

Ila nmb hawana mashart ya kingese. Crdb ilikuwa niuze deni benk ingine, jamaa wanakataa kata kata, nikasema one, nikaachana nao. Mkopo huo wa 50m utalipa si miaka 9 tu, crdb ni benk ambayo ingeendelea kitambo, tatizo ni urasimu.

Yaan hata kadi yao nimeichoma moto
Hio bank sijawahi ipenda

Sijawahi kuwa mteja wao.

Juzi kati nilienda kulipia land fees mahali Fulani

Sasa nikazunguka mawakala wote NMB wanasema hawana flot.

Benki ya NMB haipo karibu ikabidi tu niingine hapo CRDB kwanza nilikutana na mdada mkaksi vibaya utadhani benki yake.

Sidhani kama nitakuja gusa hio benki.

Benki zangu ni NMB, EQUITY na ABSA tu.
 
Mkopo ni mzuri na mkopo unainua sana km ukiwa na marengo na mipango yako ikienda vile umepanga

Kwa ufupi mkopo ukusogeza karb na mafanikio
Ila usije tafta ushauri kwa watu usowajua
Million90 ni nying sana ebu jarb kutafta watu wako wa karb wakupe ushauri
 
Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Usichukue huo mkopo kwasababu akili zako bado ni duni kwenye hayo mambo na tayari afisa mikopo kashakuingiza mkenge. Hapo utalipa 80% ya hiyo 50m kama Riba. Hiyo 16% uliyotajiwa ni lugha tamu ili uone ni rahisi. Utakuwa unarudisha 833,333/= kila mwezi kwa muda wa miaka 9. Business plans zote ni nzuri kabla ya implementations kwahiyo ninakushauri kama ni kuanza biashara anza kidogo kidogo kwa kiasi ulicho nacho mkononi. Achana na hiyo mikopo ya muda mrefu.
 
Mkopo wenye Riba hauna baraka...utakufelisha tu mbelen

Kama kazi ndio dhamana na ukishindwa kulipa hakuna kitu chako binafsi kitaathirika, Beba fuba hilo mkuu.

Maisha haiahitaji kusita. Hapo najua utakatwa na kidogo kitabaki kuendeshea maisha.

Kama uko bize sana, Jengea nyumba hakikisha unakuwa na hati kabisa, hata wakijichanganya unaingia tena kwingine hiyo nyumba inakuwa ndio collateral unavuta fuba tu. Usiogope.
Kazi ndiyo dhamana Mkuu
 
Kazi ndiyo dhamana Mkuu
Za hivyo huwa tunachukua tu mzee baba. Risk free. Beba fubq hilo w4ka mipango, ikifeli maisha hayasimami unasonga mbele.
Kama uko bize jengea tu.

Kuna mtu nimekutana nae anachukua mkopo wa kulipwa miaka 50, anakopea kwa ajilo ya shule yake zaidi ya B. Sasa miaka tisa tu sio kitu. Hata ukiingia pori ukapanda miti ya pines kwa nidhamu siku unamaliza miaka 9, unauza milioni 90+ wakati wewe unakuwa umetumia kama30 tu.
 
Hii pesa nataka nikainvest Kwenye mutual fund ambapo interest yake ni compound interest
Chukua mzigo invest huko faster.
Hadi inafika miaka 9 akili itakuwa imeshafanya mengine mengi. Hauchukui hiyo alafu aunakufa. Bado harakati zitakuwa zinaendekea na unaweza kubarikiwa kwa mengine zaidi ikiwemo hata promotion kazini ambayo itafuta machungu ya makato.
 
Back
Top Bottom