Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Kuwekeza si biashara pia maana ndio amesema hivyo
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?

Msimsingizie. Yeye huenda mpango ni starehe tu.
 
Mkuu sio Kila anaechukua mkopo ni kapuku
Kweli mkuu nimekuelewa ila mkono umetereza kwa majibu ya mdau mmoja hapo
Nao kila anae comment humu wanadhani njaa zimemleta hapa

Yaani forums za wenzetu ni tofauti kabisa na ya kwetu kwani wao wanaulizna na kujibiana tu na kama hata mtu akisema ndege yangu imepata hitilafu huwezi ona mtu anabeza bali watamuuliza ni aina gani ya ndege

Sasa njoo humu ukosema nina baiskeli wanakuambia huna hadhi ya baiskeli wakati hajui kama uko Vietnam au malagarasi
Umasikini wakati wote ni shida tu daa
 
Sijawahi kuchukuwa mkopo wala baba yangu hajawahi kuchukua na alikuwa na biashara zake Tatu akianza akiwa na miaka 20 tu
Mimi nimefanya kazi ya kuajiriwa sambamba na biashara na sijawahi kuchukua mkopo

Leo nina miaka zaidi ya 60 na nina uwezo wa kununua hata nyumba kubwa ya 200m bila shida yoyote na ni cash
Mimi sio masikini hata familia yote

Ila ukitaka uwe na nidhamu ya hela save sana bila kutegemea mkopo, achana na mwenye mamilioni huyo huwezi kujua amechukua mkopo kwa mkataba wa aina gani na aliempa

Mimi naweza kumpa mtu mkopo wa bila riba kwa sharti la kurudisha baada ya mwaka mmoja, na ndio nafanya na ndugu zangu

Nilichukua mkopo wa mwezi mmoja wa 80m nilipopata dili la chap chap na nikatengeneza 20m kwa wiki 3
Nilimrudishia mshkaji wangu 80 yake bila senti ya ziada na kumuambia nimepata 20m profit
Hapo hatuna riba na maisha yanaenda boss

Sio sifa wala nini bali haya ndio maisha yetu kiuhalisia
Uwe na siku njema
Wewe una zaidi ya miaka 60?
 
Attachments

  • 20231021_151712.jpg
    20231021_151712.jpg
    48.4 KB · Views: 8
Nunua Bajaji 7, Kila siku Hesabu 15,000/- x 7= 105000 per month ni 3,150,000/- toa marejesho 833,000/- au Tena unaweza ukalipa marejesho Mara 3 ie 2499000
 
Nunua Bajaji 7, Kila siku Hesabu 15,000/- x 7= 105000 per month ni 3,150,000/- toa marejesho 833,000/- au Tena unaweza ukalipa marejesho Mara 3 ie 2499000
1. Kwanza kabisa hajaomba ushauli wa biashara gani afanye. Yeye ameuliza tu achukue mkopo au aache!

2. Naona mchanganuo wako ni faida tupu. Hasara wapi? Una uhakika gani kama zitatembea miezi hata mitatu? Kila siku? Hilo halipo
 
Wewe una zaidi ya miaka 60?
Kwani tulisoma wote?
😄 humu hatujuani na kuna watu wa kila aina ndio maana huwa nasema ukizoea uongo kila mmoja unamuona muongo muongo tu

Ndio nina zaidi ya miaka 60 kwani niliondoka bongo nikiwa kijana wa miaka 20 kama miaka 40 na kitu iliyopita
Vita vya uganda nilikuwa nimeisha maliza form 4

Sidanganyi na huu ndio uhakika wenyewe kwani sipati zawadi ya kuwa mzee au sio
 
Chukua mwanangu, alafu toa 10M katengeneze Tent za kukodisha 5, kwa mwaka jiwekee kurudisha mkopo kwa kiasi cha 10M ndani ya biashara zako tu. Tent pekee kwenye hio 10 zinakupa 5M, hio 5M nyingine angalia 40M utaiwekeza wapi.
Biashara ya tents kwa sasa maeneo mengine imeingia mdudu.

Mfano hapa mtaani kwangu "wanazengo" tumechangishana na kununua tents na viti vyetu ni free ukiwa na shughuli yako.

Kanisani napo "kigango" chetu tumechangishana kuna tents ukiwa na shughuli utalipia usafiri tu ila asiyemuumini ndiyo anatozwa.

Katika mazingira yangu,hiyo biashara tayari ni kichaa.
 
Mkuu mimi nafuatilia comment za wadau maana nami ni mdau mkubwa wa haya mambo. Namna ulivyoandika weqe ni rahisi sana ila kiuhalisia unadhani ni issue gani ya kukupa faida hiyo per day
Zipo nyingi sana chief Cha muhimu ni consistency tu kwenye jambo lako maana mwanzoni hua ni pagumu mpaka u colonize territory yako ndio hio laki per day inakua kama buku tu
 
Biashara ya tents kwa sasa maeneo mengine imeingia mdudu.

Mfano hapa mtaani kwangu "wanazengo" tumechangishana na kununua tents na viti vyetu ni free ukiwa na shughuli yako.

Kanisani napo "kigango" chetu tumechangishana kuna tents ukiwa na shughuli utalipia usafiri tu ila asiyemuumini ndiyo anatozwa.

Katika mazingira yangu,hiyo biashara tayari ni kichaa.
Ni muono wako, hamna shida. Unadhani ni jamii ngapi Tanzania wanaweza kufanya kitu mlichokifanya nyinyi..?
 
Kweli mkuu nimekuelewa ila mkono umetereza kwa majibu ya mdau mmoja hapo
Nao kila anae comment humu wanadhani njaa zimemleta hapa

Yaani forums za wenzetu ni tofauti kabisa na ya kwetu kwani wao wanaulizna na kujibiana tu na kama hata mtu akisema ndege yangu imepata hitilafu huwezi ona mtu anabeza bali watamuuliza ni aina gani ya ndege

Sasa njoo humu ukosema nina baiskeli wanakuambia huna hadhi ya baiskeli wakati hajui kama uko Vietnam au malagarasi
Umasikini wakati wote ni shida tu daa
Nimekupata Mkuu
 
Back
Top Bottom