Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Nenda Azania bank riba ipo chini 14%
 
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Wacha kuogopa. Hiyo 40,000,000 ni kubwa kitarakimu. Ila kwa muda waliokupa ni sawa. Maana yake unarejesha wastani wa shilingi 375,000 kwa mwezi au shilingi 12,500 kwa siku. Kitu ambacho kinawezekana. Angalizo langu. Kama unauchukua huo mkopo uwe ni biashara endelevu,ambayo unajua faida na changamoto zake. Lakini kama ni biashara ya kuanza. Mhh kalagabhaho
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitat
 
Niliconsider na Muda pia nikaona ingekua better kama ningechukua mkopo mkubwa niuwekeze now kuliko kuchukua mdogo....niliona Io 50M nkiwekeza now after 4 yrs itakua imezalisha sana ...ila riba ndo ikanitoa stimu naona bank watafaidika sana
Naoaga mkopo wa miaka mingi una riba ndefu sana ni bora uchukue wa muda mfupi wenye riba ndogo huku ukiangalia progress ya jambo lako.
 
Mimi kama mchumi nakushauri chukua mkopo wa kati ya miaka miwili na mwaka mmoja utatembea vizuri sana. Kwa hiyo hesabu hapo maana yake wewe unaweza kupata milioni 9 kwa mwaka. Kisha baada ya mwaka unakopa tena tisa kwa mika 9 utakuwa umekopa 81m. Kama ni biashara au mradi utakuwa umetanuka sana.
 
Nimeishi,nime experience uchawi kwenye biashara chief. Una haki ya kusema ni ujinga kutokana na experience za lifestyle yako lakini sio kuleta outright dismissal ya hoja yangu.

Anyway kwa pesa hiyo mdau anaweza kuagiza truck ya gazeti toka South Africa kwa m36 kila kitu. Huko Tz atauza 45-49 m kwa mzigo wote ndani ya siku 30. Pia kuna biashara ya mafuta kama vaseline,Nivea lotion/deodorant, kuagiza pombe Kali nayo ni big money.

Kazi za kufanya zipo lakini ibada,matambiko au ndumba za ulinzi muhimu. You must be strong spiritually kwenye harakati za utafutaji
Hii ya magazeti mpyaa sijawahi isikia lakini nimekuwa nikiona magazeti ya shoprite na pik and pay bongo najiuliza hii vp tena???kumbe ni mchongo
 
Tuscano Vuta mkwanja wangu,... Rejesho likisumbua sumbua....nione!

Maana miaka 9 ni mingi .... Njoo nikupee odds 5 🏀 tu za kikapu!... Uwarudishie pesa yao chap!!! Na uwasahau mazima!

Na uachane nao mazima kiroho safi...

Ingawa najua benki watakutafuta tena...wakupe kopo jingine tena!...

Maana benki zilivyo na Nye. ge za kupenda pesa!...wanapenda vya bwerere! Wazee wa kudabo... Sijui huwa wanadhani hizo hela za kudabo huwa mtu unaziokota! !?
 
Ahsante Mkuu ..huu mkopo sifanyii biashara...nataka nikauwekeze kwenye mutual fund ninufaike na compound interest
Mh..hiyo kali
Kweli mkuu nimekuelewa ila mkono umetereza kwa majibu ya mdau mmoja hapo
Nao kila anae comment humu wanadhani njaa zimemleta hapa

Yaani forums za wenzetu ni tofauti kabisa na ya kwetu kwani wao wanaulizna na kujibiana tu na kama hata mtu akisema ndege yangu imepata hitilafu huwezi ona mtu anabeza bali watamuuliza ni aina gani ya ndege

Sasa njoo humu ukosema nina baiskeli wanakuambia huna hadhi ya baiskeli wakati hajui kama uko Vietnam au malagarasi
Umasikini wakati wote ni shida tu daa
Hiyo ni kweli ...wabongo tuna nongwa sana mimi huwa napiga fix Quora digest na wazungu wanamwaga ushauri kama wote njoo humu sasa unasema ukweli unaitwa muongo.
 
Mh..hiyo kali

Hiyo ni kweli ...wabongo tuna nongwa sana mimi huwa napiga fix Quora digest na wazungu wanamwaga ushauri kama wote njoo humu sasa unasema ukweli unaitwa muongo.
Tatizo ni sehemu uliokulia kama ni sehemu wengi waongo na kusema ukweli ni mwiko kwao basi wanakuwa waongo mpaka wanazeeka na ukweli pia wanaona uongo tu

Kuna mtoto alikuwa anaongeea na mwenzie walikuwa na umri wa kati ya 8 na 10
Mmoja anamwambia mwenzie aise baba ni muongo sijapata kuona 😄
Nikasema nifanye uchunguzi kuhusu hilo na ninamjua baba yake
Jamaa siku moja akapokea simu anaulizwa uko wapi akasema safari wakati kakaa sehemu mji huo huo

Mswahili hata ukifanya nae biashara unataka kitu kwake akisema Laki we mwambie Elfu kumi uone atapunguza ngapi
Utaondoka umelipa elfu 40 hao ndio wabongo
Mkuu mitandao na wenzetu ni facts tu huwezi kuta mtu anakuita muongo
 
Mimi kama mchumi nakushauri chukua mkopo wa kati ya miaka miwili na mwaka mmoja utatembea vizuri sana. Kwa hiyo hesabu hapo maana yake wewe unaweza kupata milioni 9 kwa mwaka. Kisha baada ya mwaka unakopa tena tisa kwa mika 9 utakuwa umekopa 81m. Kama ni biashara au mradi utakuwa umetanuka san
 
Back
Top Bottom