Ninatoa dollar $1000 kwa atakaenifanikishia Visa hii

Niombe msitiririke sana, mkamuone huko PM, huenda beberu wanasomewa hizi mbinu adhimu na vibaraka wao.

Wazamiaji tukadakwa kiulaini na makabrasha na suti za kuazima za kuombea visa!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hawajaondoa Hilo zuio bado ila kwa taarifa nilizonazo wameanza kulegeza masharti huko kwao hivyo Kuna matumaini kuwa mpaka kufikia Mwezi kesho katikati huenda wakaondoa Hilo zuio
 
Umesema ukweli kabisa hata mimi nimeambiwa hivi hivi na anaenialika nisitumie vichochoro kwani itanigharimu, mi nimeuliza tu gharama ya kupata visa ya UK ili nipate picha ya gharama zake zilivyo

Nashukuru Sana kwa hii comment kwangu itakuwa kama tahadhari hasa Kama mtu unategemea kwenda kwenye nchi za watu, ubongobongo tuuache huku, huko haitakiwi kabisa
 
Sasa kama hii ndefu "War and Peace" utaweza kusoma?

Unaweza kukuta chini kuna zawadi kubwa ya hela umeikosa kwa uvivu wa kusoma tu.
Hamna huwa sisomi upumbavu tu! I'm addicted to it.
Thank you enjoy your day kiranga, you can mind your business. Mr Right.
 
Niombe msitiririke sana, mkamuone huko PM, huenda beberu wanasomewa hizi mbinu adhimu na vibaraka wao.

Wazamiaji tukadakwa kiulaini na makabrasha na suti za kuazima za kuombea visa!

Everyday is Saturday............................... 😎
Wewe Ni mwanaume! Wanaume tunapambana hadi kieleweke!. [emoji41][emoji16]
 
Watu waliokaa ughaibuni miaka mingi wanajua kwamba kutumia njia za mkato kuna gharama sana.

Unaweza kufanikiwa kwenda ughaibuni halafu kwa sababu umeingia kwa njia za mkato ukashindwa kutoka.Unaitwa nyumbani kwenye harusi na misiba unashindwa kutoka huko ughaibuni, unaogopa ukitoka huwezi kurudi tena na hapo ushakaa miaka mingi ushajenga maisha yako huko.

Kuna maneno mengine nikiandika mtu hawezi kuelewa mpaka na yeye aje huku akae.

Ni bora mtu akapata visa ya halali tu, kitu ambacho si kigumu hivyo, mbona watu wanapata kila siku?
 
Hamna huwa sisomi upumbavu tu! I'm addicted to it.
Thank you enjoy your day kiranga, you can mind your business. Mr Right.
Wewe sizitaki mbichi hizi umeniita mwenyewe hapa kuniomba msaada, nimekusaidia unaita msaada wangu wa mawazo upumbavu kwa sababu umepata mtu wa kukuambia ukweli ulio tofauti na unavyotaka wewe.

Huko Ulaya unakotaka kwenda hupawezi wewe, kwa sababu kama unashindwa kukubali kuambiwa ukweli hapa JF, huko utakutana na watu wana midomo michafu wanakuambia ukweli wao wewe nyoronyoro utaona kama wanakutukana.

Halafu ukiangalia kushoto hakuna mjomba, kulia hakuna shangazi. Lazima utalia kikwenu wazungu wanakubagua.

Kumbe wanakupa za uso kwa ukweli na uwazi wao tu.

Kama hujaweza kukubali maisha ya kuambiwa maneno tofauti ya ukweli mchungu na watu tofauti, maisha ya ughaibuni hutayaweza.
 
Muhimu Ni kuwa mvumilivu tu maana vya halali vinachukua muda mrefu kukamilika hapo ndipo unakuta raia tunatafuta shortcut ambayo badae inatugharimu vibaya, wacha niwe na subira
 
Ukitaka Visa kwa urahisi uwe na angalau $3500 iyo elfu moja yako bado Sana ongeza pesa mkuu.
 
Mkuu Kiranga ana haki ya kusimamia kile anachokiamini, however, sio kila mtu ana a picture perfect scenario. Hawana hizo bank statements, elimu au skills za kuwafanya wapewe visa kirahisi kwenda nje ila nao wanataka kwenda huko.

Hapo ndo unakuja uchakachuaji. Kila kitu kinawezekana kwa mlango wenyewe au mlango wa nyuma. Katika kupita mlango wa nyuma lazima mtu uchukue calculated risks na ujue exactly what could happen should things backfire.

Aidha, japo huwezi kupata a counterfeit visa unaweza kutumia counterfeit documents kupata hiyo visa. Docs kama Bank statements, uthibitisho wa ajira, mali zinapatikana hasa bongo yetu hii. Hata muhuri wa Ikulu unapata dare I say it.

Kama unataka kwenda kwa njia ya shule basi huna budi ku-apply kwenye hiyo shule ili upate admission letter. Ni kazi yako kuapply chuo unachoona kina masharti nafuu kwako.

Mwisho, usiende kwenye nchi ya watu kwa njia ya kuzamia hapa naongelea zile njia za kuingia bila passport wala visa. Hapo utakua unajichimbia shimo kubwa zaidi. So long as umeingia kupitia a port of entry basi utatoka tu.

LaRosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…