Hata kama tunataka kusaidiana kufikisha malengo, kusaidiana kwa kufuata njia zilizowekwa ni kuzuri kuliko njia za panya.
Yani hata kama unafanya makaratee na masarakasi, unatakiwa kufanya hayo makaratee na masarakasi kwa akili mpaka serikali inapojua unafanya makaratee ishindwe kukufanya lolote, kwa sababu unayafanya ndani ya sheria zilizowekwa!
Mimi niko viwanja vikubwa nimeingia kwa njia za kueleweka nafurahia maisha, sijawahi kuwa out of status hata kwa sekunde moja mpaka nimechukua uraia wa Mnyamwezi.
Naona watu wanavyohangaika kila siku kwa sababu tu hawakufuata njia zinazoeleweka, watu wamesoma wanafanya kazi ziko chini sana ya uwezo wao, watu wanafiwa na wazazi wao wanashindwa kurudi Africa kuzika kwa sababu wakiondoka hawana uhakika wa kurudi tena ughaibuni, watu wanaishi kinyemela nyemela kwa unyonge sana, hata wakifanyiwa uonevu hawawezi kushitaki kwa kuogopa kuwa deported.
Kwa hiyo hizo njia mnazoona shortcut ndiyo kiuhalisia zinaweza kuwa ndefu zaidi katika maisha, na hizo njia mnazoona ndefu ndiyo zinaweza kuwa na manufaa zaidi.