Ndiyo maana nikasema kwamba nimepata tabu sana kuujibu uzi huu, na nilikataa kuujibu nikawa napewa tags kuujibu.
Nilijua kwamba nikiujibu ni lawama (majibu yangu hayataeleweka kwa wengine) na nisipoujibu ni lawama (Kiranga tunamuita ajibu na kusaidia kwenye uzi anaringa).
Ila ukae ukijua kitu kimoja, mimi siko hapa ili wewe unione mtu mzuri sana.
Ukinitag kutaka maoni yangu, nakupa maoni yangu.
Na siogopi kuonekana mpumbavu, naogopa kuogopa kuonekana mpumbavu.
Nimetoa majibu kwa hoja, umerudi kunishambulia kwa kitu kinachoitwa "ad hominem" kwa kilatini.
An ad hominem attack, yani, kuacha kujibu hoja za mtu na kuanza kumshambulia mtu mwenyewe kibinafsi, ni attack fulani za watu mufilisi wa hoja ambao wameshindwa kujadili hoja wanatukana mtu.
Sasa mimi kusema sitaki kumsaidia mtu kusafiri nje kwa njia za mkato, kwa kuwa njia sahihi zinajulikana nimefanya kosa gani?
Au mimi kusema sipendi watu wanaotumia fedha kupindisha utaratibu nimekosea nini?
Au mimi kusema sitaki kusaidia rushwa na hadaa nimekosea nini?
Au mimi kusema siku hizi kuna watu wengi wanafanya uhalifu wa biashara za madawa ya kulevya na ugaidi, na hivyo kumsaidia mtu nisiyemjua ni jambo hatari nimekosea nini?
Jifunze siku nyingine usiwa tag watu kuwaomba msaada katika mambo ambayo hawayafagilii, wasije kukukatalia halafu ukawalaumu wao kwa kusimamia misimamo yao na kukueleza kuhusu misimamo hiyo, wakati umewaomba msaada wewe mwenyewe.
Wewe unataka nikufuate inbox wakati wewe hujanifuata inbox, sawa hiyooo?
Haaaaaata, hiyo si sawa LaRosa, wacha vitukoo.