KNICKPOINT
New Member
- Feb 13, 2013
- 2
- 0
Nilikutana na binti mmoja chuoni nikampenda sana na yeye alinipenda tukamua kuwa wapenzi na kwakuwa alinipenda,ilimbidi aniweke wazi kwa kila kitu.Aliniambia alikokuwa alikuwa na mpenzi wake ila waliachana baada ya kubaini kuwa mpenzi wake huyo hakuwa mwaminifu.Kwa furaha kubwa niliendelea kuwa nae kama mpenzi wangu bila kumshuku kwa lolote. Lakini cha ajabu alikuwa makini sana na simu yake ya mkononi na kila nilipo jaribu kumuomba aliniuliza aliniuliza swali kwamba? nataka simu ya nini?.Siku zilivyozidi kwenda nilijabaini kuwa bado alikuwa na mahusiano na yule mpenzi wake,na nilipojari kumuuliza alinijia juu kwa ukali akisi kwamba ugomvi ulioibuka ulisababisha tukaachana. Tulipochana mimi nilishindwa kuendelea kuishi bila mpenzi nikajikuta nampenda binti mwingine wa mwaka wa kwanza ambaye na yee alinipenda tukaamua kuwa kuishi kama wapenzi na ndiye ninayeendelea naye hadi sasa.Yule mwingine naye hakuweza kuishi peke yake chuoni japo anampenzi mwingine nyumbani kwao, amejikuta wanapendana na mwanachuo mwingine wa mwaka wake japokuwa wakati kabla sijaachana nae aliapa akasema,''endapo itatokea akaaachana na mimi kamwe hataweza kuwa na mwanamume mwingine katika mazingira ya chuo kwa kuwa hakuna anaye mfaa.'' TATIZO nililo nalo ni kwamba?kwakuwa nilimpenda sana ninapat shida sana moyoni hasa pale ninapomuona chuoni na mbaya zaidi akiwa na mtu mwingine napata shida sana japokuwa huyu niliye naye ananipenda sana.NAOMBA USHAURI WENU.Nifanye nini niweze kuiepuka hii hali.Japo katika kipindi nilicho kuwa naye sikuwahi kukutana nae kimwili,lakini naumia sana nimuonapo.