Mnaweza kujadili vile mnavyofikiri kwa sababu ya hizo sadaka lakini mnasahau kuwa kuwa mchungaji hakuondoi mahitaji ya kibinadamu, wanahitaji kusomesha Kama unavyosomesha wewe, wanahitaj kukaa mahali pazuri Kama unavyopambana wewe ukae mahali pazuri
Wakati Mungu anagawa urithi kwa wana waisrael kabila la lawi hawakupata urithi wowote, wao walitakiwa wale vile vinavyoletwa madhabahuni na hao ndugu zao maana wao kazi yao ilikuwa kutumika madhabahuni hawakupaswa kulima au kufanya kazi yoyote ya kiuchumi, kwahiyo walitakiwa kuishi kutikana na hizo sadaka. Sasa mtu unaposema mchungaji ameenda kuhubiri asipewe chochote kwa sababu amehudumiwa unatakiwa kujiuliza alienda na familia yake??... Lakini maandiko yanasema mtenda kazi astahili posho lake.
Hebu tutafakari hapa unamgonjwa ukaenda kumfuata mtumishi amuombee akapona kwani hutakiwi kumshukuru Mungu?? Na ukimshukuru kwa sadaka atachukua nani Kama sio huyo mchungaji aliyekuja?
Huko kwa manabiii mnayataka wenyewe kwenda kupigwa kwasababu nabii huwa hajitangazi anayejitangaza ni tapeli.
Kingine unapotoa sadaka imani yako unaiweka wapi kwa Mungu au kwa anayepokea sadaka yako? Unapotoa sadaka weka imani kwa Mungu usiweke imani kwa anayepokea kwa sababu sadaka haziend mbinguni zinatumika hapa hapa katika kufanya kazi ya Mungu.
Hitimisho huwezi kutumia sadaka kumtambua mchungaji wa kweli au asiye wa kweli mbona kwa waganga mnapeleka sadaka na hamuwalalamikii kwa utapel wa kupokea sadaka?? Bibilia inasema mtawatambua kwa matendo yao.
LINDA SANA IMANI YAKO, KWA SABABU MCHUNGAJI, NABII AU MTUME HANA NAFASI YA KUKUTETEA BALI MUNGU NDIYE ATAKUTETEA