Ninaunga mkono kutumbuliwa kwa kiongozi mwandamizi tuliyedokezwa na mbunge Sumai

Ninaunga mkono kutumbuliwa kwa kiongozi mwandamizi tuliyedokezwa na mbunge Sumai

Mkitumbuana kwenye vikao vyenu huko mnaonaje yakibaki huko huko.

Maana Polepole mlivyompoteza hadi leo hakuna mlichokisema mlikaa kimya, hivyo hata huyo Yuda shughulikeni na yeye kimya kimya msituletee kelele zisizo na tija.

Na huo muda unaotaka huyo mama aongezewe hadi 2037 ni awe yaya au matron hapo nyumbani kwako?
 
Mimi naona lilikuwa jambo la kichama zaidi na kutakiwa kuwasilishwa kwenye vikao vya chama. Ila Simai ana hoja ingawa alitumia platform isiyo sahihi. Kwa aliyoongea ni wazi italeta maneno mengi ndani ya chama na kuchafua hali ya hewa.

Kama mtu ninayetaka mama aongezewe muda wa kuongoza hadi 2037 ninamuunga mkono Simai kuwa kama kuna kirusi ndani ya serikali kidhibitiwe mapema sana. Ni sahihi kumtumbua huyo kiongozi anayeleta shida. Kama hawezi kwenda sawa na maono ya mama akae pembeni na kuwapisha wanaoweza kufanya kazi chini ya mama.

Kuna wapuuzi wasiojua vizuri madaraka ya Rais na mwenyekiti wa CCM wanaojiaminisha kuwa kuna mtu ndani ya serikali na CCM anaweza kuzinguana na Rais akashinda hiyo battle. Ninamshauri huyo aliyetajwa na Sumai kuomba radhi mapema sana offline kabla ya kujikuta akitembea kwa magoti kutoka mlango wa Ikulu hadi ofisini kwa Rais na asisikilizwe.
Wee nae kidampa tu unahangaika humu upate angalau buku saba then unaleta propa G za kijinga!!
 
Back
Top Bottom