Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Leo nimeamua kuwapongeza CHADEMA kwa kuonyesha weledi wa kisiasa kwa kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria ya uchaguzi. Safari hii ufipa wamejitahidi tofauti na wakati mwingine.

Hata kama sikubaliani na maoni yao yote ila nakubaliana na namna walivyojitahidi kupanga hoja zao.

Nawapongeza pia kutoruhusu kila kada wa Ufipa na kupost maoni kwenye social media hali inayofanya CHADEMA ionekane kama familia ya kambale kila mwanafamilia ana ndevu.

Imezoeleka huko UFIPA kila mtu ni msemaji wa chama. Pia nakipongeza ACT kwa kuwafundisha CHADEMA siasa za kisomi. ACT wao hutoa matamko yao kisomi na sio kila mwanachama kuropoka mitandaoni.

Maoni mengi sio mabaya kwa kutolewa na chama cha siasa kinachotaka kushika dola ingawa maoni mengi ni copy & paste toka kwenye rasimu ya Warioba. Mimi nimeshangazwa sana na hoja namba 5 inayosomeka hivi:

"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".

Hii ni hoja ambayo haikutakiwa kutolewa na chama kinachojinadi kuguswa na mzigo wa kodi walio nao wananchi kugharamia uendeshaji wa serikali. Yaani kwenye hizi zama tunazotaka wabunge wapungue kutoka 393 hadi labda 100 wao CHADEMA ndo wanataka waongezeke wengine? inashangaza na kutia hasira mno.

Wabunge wa kuchaguliwa mwaka 2020 walikuwa 264 kwahiyo kwa hesabu za hovyo za Ufipa wanataka waongezeke wengine 264. Hoja yao hii ikipita tutakuwa na wabunge zaidi ya 528 kwenye bunge lijalo. INAKERA SANA kuwa na upinzani unaowaza jinsi gani waingie madarakani na kutafuna kodi za wananchi.

Ninashauri hoja za CHADEMA zisomwe kwa utulivu mkubwa kwasababu kuna hoja zina nia ovu kwa mwananchi mlipa kodi. Hoja zao zimejikita kushika dola zaidi bila kujali maumivu atakayopata mtanzania.

Pia wanaCCM na wazalendo tusichoke kukiadhibu hiki chama cha Mbowe kila fursa ya sanduku la kura inapojitokeza. Kuanzia ngazi ya kitongoji lazima tukiadhibu CHADEMA.
Mkuu

Nakuunga mkono kwa hoja hii haina tija ni utapeli na mwanya wa kuwanyonya wananchi kupitia wawakilishi wanaoenda bungeni kujitajirisha na hawana msaada wowote kwa wapiga kura
"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".

HAIFAI na CDM wanatakiwa waombe radhi kwa wananchi haraka iwezekanavyo
 
Ndio rasimu ya warioba ndio ilisema bungeni kuwe 50-50.
Viti maalum kufutwa.
Na majimbo kupungua hadi 50 pekee bara na 25 zanzibar.

Hawakusema majimbo yawe haya haya 100+
Hiyo rasimu nayo ilikuwa na mapungufu. Haya mambo ya 50 kwa 50 hayana maana yoyote zaidi ya kufuata agenda za mabeberu zisizo na tija.
 
Mkuu

Nakuunga mkono kwa hoja hii haina tija ni utapeli na mwanya wa kuwanyonya wananchi kupitia wawakilishi wanaoenda bungeni kujitajirisha na hawana msaada wowote kwa wapiga kura
"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".

HAIFAI na CDM wanatakiwa waombe radhi kwa wananchi haraka iwezekanavyo
CDM hawawezi kuomba radhi ni vichwa ngumu.
 
Mkuu majimbo yako 264 kwahiyo wakisema waweke huo usawa tutakuwa na wabunge 528 wa kuchaguliwa ambao ni zaidi ya hawa waliopo. Utakuwa ni mzigo mwingine mzito kwa wananchi.

Shida unalazimisha uongo. Majimbo yatapunguzwa. Jaji warioba kwenye Tume ya Katiba Mpya, alipendekeza majimbo 70 tu. Na kila Jimbo liwe na me na ke, jumla wabunge 140. Na ndio mapendekezo ya CHADEMA.
 
Shida unalazimisha uongo. Majimbo yatapunguzwa. Jaji warioba kwenye Tume ya Katiba Mpya, alipendekeza majimbo 70 tu. Na kila Jimbo liwe na me na ke, jumla wabunge 140. Na ndio mapendekezo ya CHADEMA.
Tunaongelea maoni ya CHADEMA na sio rasimu ya Warioba. Economist usikurupuke.
 
Mkuu Tindo unadhani bunge la wabunge wengi lina tija yoyote kwa taifa? Kupunguza mishahara si kitu kirahisi. Wabunge kwenye maslahi yao huungana na kuwa kitu kimoja bila kujali vyama. Kama hoja ni uwakilishi unadhani kuna mbunge gani anamzidi kuwasemea wananchi kama baadhi ya wanaharakati wa mitandaoni Malisa, Mange, na wengine? Kwa huu ulimwengu wa digital inapaswa bunge liwe na watu wachache wenye weledi.

Umedakia hoja usiyoijua. Mapendekezo ya CHADEMA ni majimbo yapunguzwe mpaka 70 kwa. Na kila Jimbo liwe na wabunge wawili pekee. Jumla majimbo 140. Tatizo unakimbilia kwenye conclusion bila kuangalia chanzo.
 
Kwa uroho wa ubunge ni kuwa hawa wanasiasa wetu wa vyama vyote wanatamani majimbo yaongezwe na sio kupunguzwa. Unachosema ni ngumu kutokea.

Ndio maana CHADEMA wamependekeza majimbo yapitiwe upya. Ina maana majimbo yapunguzwe. Tuwe na majimbo machache yenye wabunge wawili wawili.
 
Theoretically inawezekana lakini practically haiwezekani.
Hao wabunge watahitaji makazi, magari, sijui pesa ya mbunge, vishikwambi, mafita lita 1000. Ni mzigo mkubwa kwa wananchi.
Maendeleo hayaletwi na kujaza wabunge na msululu wa mawaziri. Sijui Afrika tumerogwa na nani
Na haya mambo ya kila jimbo kuwa na mgombea wa kike na kiume kuleta usawa ni ya ajabu kabisa. Watu hawachaguliwi kwa jinsia. Baadaye tutaanza sasa awepo anayewakisha wakristo na waislam.
Hata walioleta haya mawazo ya usawa wa kijinsia hawafanyi ujinga huu
Kwa upande mmoja hoja yako ni sahihi, kwamba hili swala la usawa wa kijinsia halina mantiki yoyote. Kinachotakiwa ni uwezo wa mtu na si jinsi yake. Huu ndio ubaguzi wa kinjisia kuona sex fulani ni dhaifu na haiwezi kushindana ktk mazingira ya aina moja. Hata hivyo viti maalum kwa wanawake vinatikiwa vifutwe, hili kutoa frusa sawa ya ushindani.

Lakini hoja ya Chadema haiongezi mzigo wowote wa gharama za uendeshaji wa bunge na wabunge. Wameshahuri tume huru itafute namna bora ya kupunguza majimbo ya uchanguzi na kuondoa viti maalum. Kupunguzwa kwa posho wanazolipwa wabunge pamoja na idadi ya vikao vya bunge vinaweza kuaccommodate hii hoja ya Chadema bila kuongeza mzigo wa gharama. Chukulia mfano wa majimbo ya uchaguzi kule Zanzibar, mengine yanazidiwa na kata kwa Tanzania bara ingawa hata kwa bara hakuna haja ya kuwa na utitiri wa majimbo.
 
Mkuu

Nakuunga mkono kwa hoja hii haina tija ni utapeli na mwanya wa kuwanyonya wananchi kupitia wawakilishi wanaoenda bungeni kujitajirisha na hawana msaada wowote kwa wapiga kura
"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".

HAIFAI na CDM wanatakiwa waombe radhi kwa wananchi haraka iwezekanavyo

Waombe Radhi kwa lipi? Kwa kutoa maoni. Umesoma maoni mengine na kuunganisha na Hilo pendekezo?

1. CHADEMA wamependekeza majimbo yapitiwe upya, kwa maana ya kupunguzwa.
2. CHADEMA wamependekeza Tume huru ndio iwajibike kupanga majimbo.
 
Tunataka reforms kwa meneo ila kwa vitendo hatutaki reforms. CHADEMA wameleta reforms ila watu wanajifanya kupinga, kesho wataanza kulalamika kuhusu viti maalum.
 
Idadi ya wabunge haina uhusiano na maendeleo maana hata hawa 300 hawareflect maendeleo tulio nayo. Ni mzigo tu kwa walipa kodi na kuongeza ulaji tu. Hata viti maalum ingefutwa tu ili watu haijalishi jinsia wakagombee tu kwenye majimbo.
Mkuu weka Uzi uliowahi kutaka bunge lifutwe kabisa maana halina tija.
 
Hiyo rasimu nayo ilikuwa na mapungufu. Haya mambo ya 50 kwa 50 hayana maana yoyote zaidi ya kufuata agenda za mabeberu zisizo na tija.
Agenda gani? Hapa Tanzania wanawake ni zaidi ya 50% sasa kuna kosa gani wakipewa equal footing?

Sisi Chadema tuliweka wagombea 70 wa majimboni kuwa wanawake yaani hatutaki viti maalum ndio viwapeleke bungeni but wapambanie majimboni.

So hii strategy sio ya kuleta 50-50 ya mezani bali competitive kwamba mwanamke apambanishwe na mwanaume wananchi waamue based on their competency sio jinsia.
 
Back
Top Bottom