Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Shida yako umesoma hiyo hoja bila kuiunganisha na hoja zingine.

1. CHADEMA wamesema Jimbo moja liwe na idadi kadhaa ya watu.

2. CHADEMA wamesema Tume huru iwe na mamlaka ya kuongeza ama kupunguza majimbo.

Kwa hizo hoja hapo juu Kuna mambo mawili yatatokea.

1. Tume huru inaweza kupunguza majimbo mengi.
2. Viti maalum hawatakuwepo.

Sasa ukipunguza idadi ya viti maalumu mia na kupunguza majimbo kadhaa idadi inafika.

..nawaunga mkono.

..kila nafasi iwe na mwanamke na mwanaume.

..hata RAIS awepo mwanamke na mwanaume.
 
Ni vipi kama wabunge watakuwa wengi kwa maana ya kuhudumia wananchi, kisha mishahara Yao ikapunguzwa zaidi ya nusu ya Sasa? Je wakipunguza posho za Sasa za wabunge, sambamba na kupunguza vikao vya bunge, huoni kama suala la gharama halitakiwepo. Tatizo ni hiyo kuongelea mapendekezo ya cdm, katika mtazamo wa kiccm.

Kwa taarifa yako huko uwanjani wachezaji huwa 11 Kila upande, lakini Kila team huwa na mbinu au mfumo wake wa kiuchezaji.
Madai yako umetoboa hoja🤣🤣🤣🤣😁.

Ukiondoa uchawa wa Chama huwa unakuwa na hoja mnoo

🏃🏃🏃
 
Agenda gani? Hapa Tanzania wanawake ni zaidi ya 50% sasa kuna kosa gani wakipewa equal footing?

Sisi Chadema tuliweka wagombea 70 wa majimboni kuwa wanawake yaani hatutaki viti maalum ndio viwapeleke bungeni but wapambanie majimboni.

So hii strategy sio ya kuleta 50-50 ya mezani bali competitive kwamba mwanamke apambanishwe na mwanaume wananchi waamue based on their competency sio jinsia.

..kwanini tunawawezesha kwenye ubunge peke yake?

..au kwanini ni kwenye nafasi za kisiasa peke yake?

..kwanini hatuwawezeshi kwenye maeneo mengine?
 
Umedakia hoja usiyoijua. Mapendekezo ya CHADEMA ni majimbo yapunguzwe mpaka 70 kwa. Na kila Jimbo liwe na wabunge wawili pekee. Jumla majimbo 140. Tatizo unakimbilia kwenye conclusion bila kuangalia chanzo.
Ni wapi kwenye mapendekezo wamesema hivi?
 
Leo nimeamua kuwapongeza CHADEMA kwa kuonyesha weledi wa kisiasa kwa kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria ya uchaguzi. Safari hii ufipa wamejitahidi tofauti na wakati mwingine.

Hata kama sikubaliani na maoni yao yote ila nakubaliana na namna walivyojitahidi kupanga hoja zao.

Nawapongeza pia kutoruhusu kila kada wa Ufipa na kupost maoni kwenye social media hali inayofanya CHADEMA ionekane kama familia ya kambale kila mwanafamilia ana ndevu.

Imezoeleka huko UFIPA kila mtu ni msemaji wa chama. Pia nakipongeza ACT kwa kuwafundisha CHADEMA siasa za kisomi. ACT wao hutoa matamko yao kisomi na sio kila mwanachama kuropoka mitandaoni.

Maoni mengi sio mabaya kwa kutolewa na chama cha siasa kinachotaka kushika dola ingawa maoni mengi ni copy & paste toka kwenye rasimu ya Warioba. Mimi nimeshangazwa sana na hoja namba 5 inayosomeka hivi:

"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".

Hii ni hoja ambayo haikutakiwa kutolewa na chama kinachojinadi kuguswa na mzigo wa kodi walio nao wananchi kugharamia uendeshaji wa serikali. Yaani kwenye hizi zama tunazotaka wabunge wapungue kutoka 393 hadi labda 100 wao CHADEMA ndo wanataka waongezeke wengine? inashangaza na kutia hasira mno.

Wabunge wa kuchaguliwa mwaka 2020 walikuwa 264 kwahiyo kwa hesabu za hovyo za Ufipa wanataka waongezeke wengine 264. Hoja yao hii ikipita tutakuwa na wabunge zaidi ya 528 kwenye bunge lijalo. INAKERA SANA kuwa na upinzani unaowaza jinsi gani waingie madarakani na kutafuna kodi za wananchi.

Ninashauri hoja za CHADEMA zisomwe kwa utulivu mkubwa kwasababu kuna hoja zina nia ovu kwa mwananchi mlipa kodi. Hoja zao zimejikita kushika dola zaidi bila kujali maumivu atakayopata mtanzania.

Pia wanaCCM na wazalendo tusichoke kukiadhibu hiki chama cha Mbowe kila fursa ya sanduku la kura inapojitokeza. Kuanzia ngazi ya kitongoji lazima tukiadhibu CHADEMA.
Bado hujasema,muda ukifika utasema tuu maana cdm ni sawa na maji
 
Agenda gani? Hapa Tanzania wanawake ni zaidi ya 50% sasa kuna kosa gani wakipewa equal footing?

Sisi Chadema tuliweka wagombea 70 wa majimboni kuwa wanawake yaani hatutaki viti maalum ndio viwapeleke bungeni but wapambanie majimboni.

So hii strategy sio ya kuleta 50-50 ya mezani bali competitive kwamba mwanamke apambanishwe na mwanaume wananchi waamue based on their competency sio jinsia.
Equal footing ni kugombea, kwani waliopo Bungeni wamefikaje?
Ok tuseme last time Uchaguzi uliibiwa, miaka ya nyuma vipi?
Kipindi kina Mdee wanashinda kawe walishindanishwa na wanawake wenzao?

Ni mjinga tu ndio hataona Kinachotafutwa hapo......
 
Mleta mada ni mpumbavu
Mbona inaonekana wewe ndiyo mpumbavu?

Kama ungekuwa una akili ungekosoa hoja zake na kuonesha mapungufu ya hoja yake.

Kukimbilia kumtukana mtoa hoja ni kudhihirisha huna akili ya kuelewa hoja yake, na huna uwezo wa kuonesha mapungufu ya hoja yake.
 
Ni vipi kama wabunge watakuwa wengi kwa maana ya kuhudumia wananchi, kisha mishahara Yao ikapunguzwa zaidi ya nusu ya Sasa? Je wakipunguza posho za Sasa za wabunge, sambamba na kupunguza vikao vya bunge, huoni kama suala la gharama halitakiwepo. Tatizo ni hiyo kuongelea mapendekezo ya cdm, katika mtazamo wa kiccm.

Kwa taarifa yako huko uwanjani wachezaji huwa 11 Kila upande, lakini Kila team huwa na mbinu au mfumo wake wa kiuchezaji.
Mapendekezo ya Mmawia ni.

1.Viti maalum vitolewe kabisa visiwepo.

2. Mishahara ya wabunge ipunguzwe iwe ni sh 1m .

3.Posho za wabunge zipunguzwe na kuwa sh 100k kwa siku.

4. Wapewe mkopo wa magari ya kawaida kabisa ya sh 30m.

Kusiwepo na kiinua mgongo mwisho wa term za kibunge.
 
Back
Top Bottom