Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu

Nakuunga mkono kwa hoja hii haina tija ni utapeli na mwanya wa kuwanyonya wananchi kupitia wawakilishi wanaoenda bungeni kujitajirisha na hawana msaada wowote kwa wapiga kura
"Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, moja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea".

HAIFAI na CDM wanatakiwa waombe radhi kwa wananchi haraka iwezekanavyo
 
Ndio rasimu ya warioba ndio ilisema bungeni kuwe 50-50.
Viti maalum kufutwa.
Na majimbo kupungua hadi 50 pekee bara na 25 zanzibar.

Hawakusema majimbo yawe haya haya 100+
Hiyo rasimu nayo ilikuwa na mapungufu. Haya mambo ya 50 kwa 50 hayana maana yoyote zaidi ya kufuata agenda za mabeberu zisizo na tija.
 
CDM hawawezi kuomba radhi ni vichwa ngumu.
 
Mkuu majimbo yako 264 kwahiyo wakisema waweke huo usawa tutakuwa na wabunge 528 wa kuchaguliwa ambao ni zaidi ya hawa waliopo. Utakuwa ni mzigo mwingine mzito kwa wananchi.

Shida unalazimisha uongo. Majimbo yatapunguzwa. Jaji warioba kwenye Tume ya Katiba Mpya, alipendekeza majimbo 70 tu. Na kila Jimbo liwe na me na ke, jumla wabunge 140. Na ndio mapendekezo ya CHADEMA.
 
Shida unalazimisha uongo. Majimbo yatapunguzwa. Jaji warioba kwenye Tume ya Katiba Mpya, alipendekeza majimbo 70 tu. Na kila Jimbo liwe na me na ke, jumla wabunge 140. Na ndio mapendekezo ya CHADEMA.
Tunaongelea maoni ya CHADEMA na sio rasimu ya Warioba. Economist usikurupuke.
 

Umedakia hoja usiyoijua. Mapendekezo ya CHADEMA ni majimbo yapunguzwe mpaka 70 kwa. Na kila Jimbo liwe na wabunge wawili pekee. Jumla majimbo 140. Tatizo unakimbilia kwenye conclusion bila kuangalia chanzo.
 
Kwa uroho wa ubunge ni kuwa hawa wanasiasa wetu wa vyama vyote wanatamani majimbo yaongezwe na sio kupunguzwa. Unachosema ni ngumu kutokea.

Ndio maana CHADEMA wamependekeza majimbo yapitiwe upya. Ina maana majimbo yapunguzwe. Tuwe na majimbo machache yenye wabunge wawili wawili.
 
Kwa upande mmoja hoja yako ni sahihi, kwamba hili swala la usawa wa kijinsia halina mantiki yoyote. Kinachotakiwa ni uwezo wa mtu na si jinsi yake. Huu ndio ubaguzi wa kinjisia kuona sex fulani ni dhaifu na haiwezi kushindana ktk mazingira ya aina moja. Hata hivyo viti maalum kwa wanawake vinatikiwa vifutwe, hili kutoa frusa sawa ya ushindani.

Lakini hoja ya Chadema haiongezi mzigo wowote wa gharama za uendeshaji wa bunge na wabunge. Wameshahuri tume huru itafute namna bora ya kupunguza majimbo ya uchanguzi na kuondoa viti maalum. Kupunguzwa kwa posho wanazolipwa wabunge pamoja na idadi ya vikao vya bunge vinaweza kuaccommodate hii hoja ya Chadema bila kuongeza mzigo wa gharama. Chukulia mfano wa majimbo ya uchaguzi kule Zanzibar, mengine yanazidiwa na kata kwa Tanzania bara ingawa hata kwa bara hakuna haja ya kuwa na utitiri wa majimbo.
 

Waombe Radhi kwa lipi? Kwa kutoa maoni. Umesoma maoni mengine na kuunganisha na Hilo pendekezo?

1. CHADEMA wamependekeza majimbo yapitiwe upya, kwa maana ya kupunguzwa.
2. CHADEMA wamependekeza Tume huru ndio iwajibike kupanga majimbo.
 
Tunataka reforms kwa meneo ila kwa vitendo hatutaki reforms. CHADEMA wameleta reforms ila watu wanajifanya kupinga, kesho wataanza kulalamika kuhusu viti maalum.
 
Idadi ya wabunge haina uhusiano na maendeleo maana hata hawa 300 hawareflect maendeleo tulio nayo. Ni mzigo tu kwa walipa kodi na kuongeza ulaji tu. Hata viti maalum ingefutwa tu ili watu haijalishi jinsia wakagombee tu kwenye majimbo.
Mkuu weka Uzi uliowahi kutaka bunge lifutwe kabisa maana halina tija.
 
Hiyo rasimu nayo ilikuwa na mapungufu. Haya mambo ya 50 kwa 50 hayana maana yoyote zaidi ya kufuata agenda za mabeberu zisizo na tija.
Agenda gani? Hapa Tanzania wanawake ni zaidi ya 50% sasa kuna kosa gani wakipewa equal footing?

Sisi Chadema tuliweka wagombea 70 wa majimboni kuwa wanawake yaani hatutaki viti maalum ndio viwapeleke bungeni but wapambanie majimboni.

So hii strategy sio ya kuleta 50-50 ya mezani bali competitive kwamba mwanamke apambanishwe na mwanaume wananchi waamue based on their competency sio jinsia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…