Pre GE2025 Ninawapongeza CHADEMA kwa maoni yao ila hoja namba 5 ni ya ovyo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Unashauri Nini boss?
 
Suala la wabunge kuwa wengi katika sura hiyo yaweza kuwa sawa lakini kwanini walazimishe mbunge mwanaume na mwanamke? Mbunge achaguliwe kwa uwezo wake na sio jinsia yake!
 
Unashauri Nini boss?
Kusifanyike anything ambacho kitaongeza mzigo wa kodi kwa mbangaizaji... Kwa teknolojia ya leo tunaweza kufanya mengi kwa theluthi ya watendaji...; Kupunguza zaidi the governing sector sio kuongeza.....
 
Nakubaliana na wewe, tunataka wabunge wapungue wawe hata 100 wenye tija badala ya sasa hawa wagonga meza pekee
 
Suala la wabunge kuwa wengi katika sura hiyo yaweza kuwa sawa lakini kwanini walazimishe mbunge mwanaume na mwanamke? Mbunge achaguliwe kwa uwezo wake na sio jinsia yake!
Utadhani Tanzania haina maendeleo sababu ya 50/50 kitu ambacho ni ujinga tupu
 
Hoja ya CHADEMA siku zote ni kuwa na serikali za Majimbo ambapo mikoa iliyopo itageuzwa Majimbo. Kwa hiyo wakisema Kila Jimbo hawamaanishi Majimbo haya ya Jaji Mutungi na genge lake. Mikoa 32 ikiwa na Wabunge wawili wawili jumla ni Wabunge 64 pekee Tanzania nzima. Bado unaona kuna Mzigo Kwa walipa Kodi kulinganisha na 293 wa Sasa?
 
Hapa tunaongelea muswada wa sheria ya uchaguzi na sio rasimu ya Warioba. Acha kuchepusha mada
 
Acha mambo ya kudhani hapa wakati hoja zao wamezitamka bila kudhani.
 
Kwamba Kila mtanzania analazimika kulipa corporate Tax? Au umeishiwa na hoja Sasa unaanza kutumia mabavu hoja yako ipite?
Unabisha upuuzi ukute hata TIN number ya biashara huna.
 
Umesoma rasimu ya Warioba? Nayo pia ilikuwa na pendekezo kama hilo. Majimbo yanapunguzwa sana. Mwisho wa siku bunge kitakuwa dogo kuliko la sasa.
 
Umesoma rasimu ya Warioba? Nayo pia ilikuwa na pendekezo kama hilo. Majimbo yanapunguzwa sana. Mwisho wa siku bunge kitakuwa dogo kuliko la sasa.
Hapa tunaongelea muswada wa sheria za uchaguzi au rasimu ya Warioba? Acha kuchanganya mambo.
 
Umesema kweli. Siasa ni biashara so wanaangalia zaidi maslahi yao.

Wanaoingia kwenye siasa kwa ajili ya kuwaletea watanzania ya kweli ni wachache sana na Uenda kwa sasa hayupo hata mmoja.
 
Umesema kweli. Siasa ni biashara so wanaangalia zaidi maslahi yao.

Wanaoingia kwenye siasa kwa ajili ya kuwaletea watanzania ya kweli ni wachache sana na Uenda kwa sasa hayupo hata mmoja.
Wewe mbona kichwa yako inawaza sana siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…