Mkuu pendekezo hilo wala halina shida kwa upande wa gharama. Kwa kuwa marupurupu ya sasa ya mbunge wa jimbo na stahili zake nyingine zote, vinaweza kugawanywa mara mbili ili viendane na mahitaji ya wabunge hao wawili.
Mathalani, kama mbunge wa sasa analipwa mshahara wa Tsh 12Mn, basi kupitia mapendekezo hayo wabunge hao wawili wa jimbo husika watalipwa kila mmoja Ths. 6Mn. Kwa upande wa posho z vikao kila mmoja itapaswa alipwe nusu ya kile anacholipwa mbunge wa sasa, n.k..
Kuliko kuwa na nafasi za wabunge wanawake wa viti maalum na tena wasiokuwa na majimbo ya uwakilishi wa moja kwa moja. Ni heri wapitie mchakato wa kupigiwa kura majimboni mwao ili kuweza kupima kukubalika kwao majimboni kuliko kutokana na utashi wa kukubalika kwao ndani ya vyama vyao vya kisiasa.
Ukichunguza kwa undani zaidi ubora wa pendekezo hili lenye mantiki, utaona dhahiri kuwa gharama kwa ujumla za uendeshaji wa bunge zitapungua sana, kwa kuwa hakutakuwepo tena na gharama za wabunge wa viti maalum, bali zile za wabunge wa jimbo zitabakia kuwa ni zile zile.