Ninawaza kuanzisha kitu kinachoitwa Tantech Association, naomba ushirikiano wenu

Wazo zuri, safi sana kijana. Ila nahisi kama sijakuelewa hivi, unajua kila organization inakuwaga na kiongozi. Unaweza kufafanua kidogo kuhusu suala la uongozi n.k
 
Wewe ndio nimekuelewa vizuri. Nashindwa kumwelewa anamaanisha nini, yaani anataka akusanye watu awawezeshe au vipi? Ndio maana nikawa nimemuuliza kama atakuwa anawalipa au vipi, maana hata umri naamini atakuwa ni mdogo
 
Wazo zuri, safi sana kijana. Ila nahisi kama sijakuelewa hivi, unajua kila organization inakuwaga na kiongozi. Unaweza kufafanua kidogo kuhusu suala la uongozi n.
ni kwel ulivyosema kaka..Nadhani mbeleni litafanyiwa mkakati mzuri...!
 
Em naomba toa mfano wa shughuli zitakazokuwa zinafanywa na hiyo association
utoaji wa elimu ya sayansi ya kiteknolojia kwa watu mbalimbali nchini hasa kwa vijana...

Kupata elimu na juzi mbalimbali kutoka kwa wabobezi wa sayansi ya kiteknolojia wanaotoka nchini Tanzania.

Pia itatoa nafasi kwa vijana wabunifu kuweza kuonyesh bunifu zao ambapo watapata shirikiano mbalimbali ikiwemo kupata hata mawazo juu ya kuwez kuendelea bunifu zao ili baadae ziwez kusaidia jamii...

Pia unaweza ona nimepost baadhi ya shughuli zilizoweza kuanza kufanya katika association hio kwa post iliyopita katika profile yangu.
 
Wewe ndio nimekuelewa vizuri. Nashindwa kumwelewa anamaanisha nini, yaani anataka akusanye watu awawezeshe au vipi? Ndio maana nikawa nimemuuliza kama atakuwa anawalipa au vipi, maana hata umri naamini atakuwa ni mdogo
Nope yaani ataka kuanzisha platform ya kukutanisha watu kwenye tasnia ya Tech..., kwahio kutakuwa na wataalamu watafuta ujuzi na watu wanaobadilishana mawazo..., Yaani tuseme kama ilivyo kwenye whatsapp groups, telegram groups au hili jukwaa la gadgets..., lakini huenda platform yake ikawa more specialized na ina vitu vingi zaidi kwahio labda hata wewe ukiwa na swali kuhusu simu yako au umegundua mashine ya kutumia mende kulima shamba unaweza kuingia huko...

In short its a community na ukiwa na community ni rahisi hata kuwasaidia wenye kupata funds awe wenye ideas ni rahisi kuweza kuonekana au kuwauzia wahitaji wa idea......

it's not a new concept lakini implementation na wahusika ndio itakuwa a make or break..., ndio maana nikamshauri aanze na wadau wake hapo shuleni asogee mashule mengine aingie hata vyuoni aingie kitaa kwa mafundi simu, computer n.k. (technicians) alafu watu watakaokuwa wanaingia kuchukua contents / knowledge (users) itakuwa ni hatua ya mwisho (sababu ukiwaita watu wengi waje kuangalia a half baked idea wakikuta ndivyo sivyo hawatarudi tena)
 
Aaha hapo kiasi nimeelewa
 
Mimi nilivyokuelewa

You need to create a platform inayo-deal na science and technology

Hii platform itakuwa Inawaleta pamoja wale wanaopenda kujifunza teknolonjia then na wale wanaotoa utaalamu wao hapo ktk hiyo platform


Lengo
Kukuza ujuzi wa matumizi ya teknolojia kwa vijana.


Kuuza ujuzi na kununua ujuzi.

Mimi nimekuelewa hivyo.

Mfano kifaa changu kikiwa na shida ya kiteknolojia naweza kuja katika jukwaa lako nikasaidiwa na mambo yakakaa sawa.
 
Safi kijana, soma sana and keep pushing naamini utafanya kitu kikubwa sana
thanks alot kwa kunipa hope ni moja ya force mnayonipa nizidi deeply thinking on how my idea can develop,thanks again🙏🏽
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…