Ninaweza kwenda Nairobi bila passport?

Ninaweza kwenda Nairobi bila passport?

al-baajun

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2015
Posts
283
Reaction score
209
Habari wakuu?

Nilikua nauliza ninaweza nikapenda Kenya bila passport?Nina kitambulisho Cha taifa je nikifika boda siwezi pata pass ya mda ya kuingia Kenya?

Na je basi zinazoenda Nairobi kutokea Dar ni basi Gani?

Natanguliza shukrani
 
Huwezi.. pata passport ya muda mfupi au ile kubwa..!! Usichohitaji ni visa, maana ni unaipatia ukiwa safarini
 
Unaweza kwa kutumia bodapasi, hii hutolewa kwa wakazi wa mpakani kuingia nchi nyingine. Pili unaweza ukaingia Kenya bila kutumia njia rasmi, muhimu ukivuka mpaka huko ndani tumia akili.
 
Mkuu kuwa makini sana na ushauri unao pewa kwenye jukwaa hili sio kila mtu ana fahamu na wengine wamejaribu mara moja waka fanikiwa basi wanafanya ndio sheria. Polisi wa Kenya wakikuotea wata kutoa hela mkuu tena sana tu naikiwezekana uta wekwa ndani.

Kabla ya kwenda Nairobi nenda ofisi ya uhamiaji Tanzania chukuwa pass ya mda mfupi ni 30k (beba picha za passport kama 3) then angalia kitengo cha afya pata Yellow fever card, andaa mask zako kama 5 weka kwenye basi.

Fika lumumba hapo check na Tahmeed chukuwa ticket kwenda border, hela omba mwongozo kwa konda kuchange hela yako usikubali kubadilishiwa hela kiholela utapigwa za uso, wata kuja wasomali kwenye gari mnapo fika Longido kuwasaidia kubadili hela mkiwa ndani ya basi kuelea boda hao ni salama zaidi na waminifu.
 
Yeah! Kuna njia za panya.
Jan 2023, nategemea kuwa Nairobi. Passport yangu imeisha tangu 2021.
So, ntapita njia za panya...
Kuna mkutano muhimu wa kuhudhuria...
 
Mkuu kuwa makini sana na ushauri unao pewa kwenye jukwaa hili sio kila mtu ana fahamu na wengine wamejaribu mara moja waka fanikiwa basi wanafanya ndio sheria. Polisi wa Kenya wakikuotea wata kutoa hela mkuu tena sana tu naikiwezekana uta wekwa ndani.
Kabla ya kwenda Nairobi nenda ofisi ya uhamiaji Tanzania chukuwa pass ya mda mfupi ni 30k (beba picha za passport kama 3) then angalia kitengo cha afya pata Yellow fever card, andaa mask zako kama 5 weka kwenye basi. Fika lumumba hapo check na Tahmeed chukuwa ticket kwenda border, hela omba mwongozo kwa konda kuchange hela yako usikubali kubadilishiwa hela kiholela utapigwa za uso, wata kuja wasomali kwenye gari mnapo fika Longido kuwasaidia kubadili hela mkiwa ndani ya basi kuelea boda hao ni salama zaidi na waminifu.
Asante sana mkuu kWa ushauri wako,ubarikiwe.
 
Yellow card fever lazima kuwa nayo? Je usipokua nayo?na hiyo passport temporary ni ya mda Gani?au utatumia safari moja
Yellow fever lazima kuwa nayo wata goma kukugongea passport. Uzuri ukisha ipata ina kaa mda mrefu 10 years ina hitajika nchi mbalimbali so itakusaidia kwenye safari zingine, passport ni mara moja ila naskia wamesha badili mfumo ina kwenda mwaka sasa so wakati una pewa utapata maelezo
 
passport ni mara moja ila naskia wamesha badili mfumo ina kwenda mwaka sasa so wakati una pewa utapata maelezo
Mkuu kumbe kwa sasa hiyo Emergency Travelling Document inatumika mwaka mzima sio kama ilivyokuwa zamani kuwa ukienda ukirudi unaikabidhi
 
Back
Top Bottom