Mkuu kuwa makini sana na ushauri unao pewa kwenye jukwaa hili sio kila mtu ana fahamu na wengine wamejaribu mara moja waka fanikiwa basi wanafanya ndio sheria. Polisi wa Kenya wakikuotea wata kutoa hela mkuu tena sana tu naikiwezekana uta wekwa ndani.
Kabla ya kwenda Nairobi nenda ofisi ya uhamiaji Tanzania chukuwa pass ya mda mfupi ni 30k (beba picha za passport kama 3) then angalia kitengo cha afya pata Yellow fever card, andaa mask zako kama 5 weka kwenye basi. Fika lumumba hapo check na Tahmeed chukuwa ticket kwenda border, hela omba mwongozo kwa konda kuchange hela yako usikubali kubadilishiwa hela kiholela utapigwa za uso, wata kuja wasomali kwenye gari mnapo fika Longido kuwasaidia kubadili hela mkiwa ndani ya basi kuelea boda hao ni salama zaidi na waminifu.